Mhasibu akana kutafuna Sh22 milioni

Mhasibu akana kutafuna Sh22 milioni

Na RICHARD MUNGUTI

MHASIBU katika chama cha ushirika cha Runka alishtakiwa Jumatatu kwa wizi wa Sh22.6 milioni.

Bw Lawrence Kathurima Mbaya , alikana mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bi Martha Mutuku mashtaka ya wizi wa kuweka hesabu bandia katika vitabu vya uhasibu.

Bw Mbaya alikana kati ya Juni 2016 na Desemba 20 2020 akiwa ameajiriwa kazi ya uhasibu na chama cha ushirika cha Runka Sacco Limited alikiibia Sh22,618,611.

Kupitia kwa wikili wake, mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Hakimu alifahamishwa mshtakiwa alikuwa ameshirikiana na wachunguzi wa kesi hiyo kati ya 2016 hadi juzi alipoelezwa atafikishwa kortini.

Hakimu alifahamishwa mshtakiwa aliweka hesabu za uwongo kwa vitabu vya uhasibu vya chama hicho. Mahakama ilimwamuru mshtakiwa alipe dhamana ya pesa tasilimu ya Sh3milioni.

Kesi itatajwa tena Machi 15,2021 kwa maagizo zaidi.

You can share this post!

Poleni mashabiki, yalikuwa tu majaribu ya kimwili –...

Shehena ya chanjo ya corona yafika Kenya