Dondoo

Mhubiri aliyehamishwa apigwa breki kuuza mahindi ya kanisa

Na DENNIS SINYO June 24th, 2024 1 min read

PASTA aliyekuwa amepata uhamisho alipata ugumu kuyauza mahindi ya kanisa baada ya kamati kuu kupinga hatua hiyo.

Inasemekana mhubiri huyo alikuwa amehamishwa ili kuchapa injili kwenye kanisa jingine baada ya kuhubiri eneo hilo kwa miaka mitatu.

Kulingana na mdaku wetu, mchungaji huyo alikuwa amepakia magunia 45 ya mahindi kwenye lori kabla ya mwenyekiti wa kanisa kufika na kuzuia lori lisiondoke.

Mwenyekiti huyo alidai Pasta huyo alikuwa amepanga kuuza mali ya kanisa bila kumweleza yeyote.

Ilibidi mhubiri huyo kuondoka bila chochote baada ya waumini kufika na kufunga nyumba yake.

Walisema kila kitu kwenye kanisa hilo kilikuwa mali ya kanisa na si mtu binafsi.