• Nairobi
  • Last Updated June 2nd, 2023 6:24 PM
AC Milan na AS Roma nguvu sawa katika Serie A huku Napoli wakifungua mwanya wa alama saba kileleni mwa jedwali

AC Milan na AS Roma nguvu sawa katika Serie A huku Napoli wakifungua mwanya wa alama saba kileleni mwa jedwali

Na MASHIRIKA

AS Roma walilazimishia mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), AC Milan, sare ya 2-2 ugani San Siro mnamo Jumapili.

Matokeo hayo yaliacha Milan katika nafasi ya tatu kwa alama 37 sawa na nambari mbili Juventus. Napoli walifungua pengo la alama saba kileleni mwa jedwali baada ya kupiga Sampdoria 2-0.

Roma ya kocha Jose Mourinho sasa inashikilia nafasi ya sita kwa pointi 31 sawa na Lazio waliotoshana nguvu na Empoli kwa sare ya 2-2. Spezia waliambulia sare tasa dhidi ya Lecce huku Salernitana wakitoshana nguvu na Torino kwa sare ya 1-1.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Covid-19: Furaha China ikifungua mipaka yake

Barcelona yazamisha Atletico na kufungua pengo la alama...

T L