• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 1:45 PM
AFC Leopards yakubaliwa kusajili wachezaji baada ya makubalianao na Aussems

AFC Leopards yakubaliwa kusajili wachezaji baada ya makubalianao na Aussems

NA JOHN ASHIHUNDU

KLABU ya AFC Leopards sasa imekubaliwa kusajili wachezaji wapya baada ya timu hiyo kufikia makubaliano na aliyekuwa kocha wao, Patrick Aussems aliyewashtaki kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Akitoa habari hizo Jumamosi, mlezi wa timu hiyo, Alex Muteshi alisema raia huyo wa Ubelgiji alikuwa akiwadai Sh20 milioni lakini kufikia wikendi hii, alikuwa amelipwa Sh12 milioni, huku wakiamriwa kumaliza deni hilo kufikai Machi 2024.

Muteshi alisema awali klabu hiyo ilikuwa imemlipa Sh8 milioni na majuzi akaongezewa Sh5 walizopewa na Serikali kupunguza deni hilo.

Leopards ilikuwa hatarini kupokonywa leseni ya kushiriki Ligi Kuu ya Kenya (FKF-PL) mbali na kuteremshwa ngazi hadi Supa Ligi (NSL) kama haingeafikiana na kocha huyo aliyejiunga na klabu hiyo mnamo Februari 2021.

“Tumekuwa na wakati mgumu kwa siku mbili zilizopita, lakini sasa tumekubaliana na tutakubaliwa kuendelea na mipango yetu ya maandalizi kwa msimu mpya,” aliongeza Muteshi.

Akieleza kuhusu jinsi hali hiyo ilivyotokea, Muteshi alisema wakati ugonjwa wa Covid-19 ulizuka na shughuli zote zikasimama, tayari klabu ilikuwa imempa kocha huyo mkataba na ilikuwa vigumu kujiondoa.

“Klabu haikuwa na pesa za kumlipa kwa sababu hata ligi ilisimamishwa na wadhamini wakakosekana. Tulifaulu kuelewana naye kwa wakati fulani na akaondoa kesi mahakamani, lakini mambo yalibadilika msimu uliopita ukielekea ukingoni,” akaeleza.

  • Tags

You can share this post!

EPL: Karen Nyamu aitakia Manchester United msimu mbaya

EPL: Saka na Nketiah wabeba Arsenal dhidi ya Nottingham...

T L