• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 2:07 PM
CAF yapokea rasmi azma ya Kenya, Uganda na TZ kutaka kuandaa Afcon 2027

CAF yapokea rasmi azma ya Kenya, Uganda na TZ kutaka kuandaa Afcon 2027

NA JOHN ASHIHUNDU

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) sasa limepokea rasmi maombi ya mataifa ya Afrika Mashariki kutaka kuandaa kwa pamoja fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Rais wa Shirikisho la Kandanda Kenya (FKF), Nick Mwendwa amethibitisha Ijumaa kwamba maombi ya Kenya, Uganda na Tanzania yamepokelewa na Katibu Mkuu wa CAF, Veron Mosengo-Omba katika makao makuu ya AFC jijini Cairo, Misri.

Kenya, Uganda na Tanzania zimeungana kuwania fursa ya kuandaa Makala ya 2027 ya michuano hiyo, hatua ambayo inaungwa mkono kikamilifu na marais wa mataifa hayo matatu – Dkt Wiliam Ruto, Yoweri Museveni na Samia Suluhu Hassan.

Mwendwa anaamini kwamba maombi hayo ya pamoja yatafaulu kutokana na umoja unaoonyeshwa na mataifa hayo yanayongojea wakaguzi wa CAF kufika kujionea jinsi hali ya viwanja vyao ilivyo.

Mwendwa amesema tayari mataifa hayo yana viwanja vya kutosha ambavyo vitahitaji tu ukarabati mdogo.

Alisema: “Qatar haikuwa na viwanja vya kutosha, lakini iliandaa Kombe la Dunia baada ya kupewa muda wa kujenga kadhaa ambavyo vilitumika kwa uandalizi huo. Mara tu unapopewa fursa hii, unaanza mara moja kujiandaa vilivyo. CAF ilitaka kuandaa mashindano ya Chan ya 2018 hapa nchini, lakini wakati huo hatukuwa tayari kama sasa.”

Mwendwa ameongeza: “Viwanja vyetu viwili vikubwa vya Nyayo na Kasarani vitahitaji marekebisho madogo sana na kukubaliwa kuandaa Afcon 2027. Tukipewa hii fursa tutahakikisha hata ule wa Kip Keino umerekebishwa ipasavyo.”

Katika maombi hayo, Kenya imewasilisha Kasarani ulio na na uwezo wa kubeba mashabiki 60,000, Nyayo Stadium (30,000) na Kipchoge Keino Stadium mjini Eldoret kama viwanja vilivyo na uwezo wa kuandaa michuano hiyo ya 2027.

Kwa maandalizi, Kenya imeorodhesha Kasarani Annex, Police Sacco Stadium, Kenya Utalii College Sports Club, Ulinzi Sports Complex na Jamhuri Sports Complex.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa wang’oa na kuteketeza bangi iliyopandwa kando...

Wakili ataka TI Kenya itoe hoja nzito za kumpokonya Haji...

T L