• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Chepng’etich ang’aria wapinzani mbio za 1500m Eugene Diamond League

Chepng’etich ang’aria wapinzani mbio za 1500m Eugene Diamond League

NA GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Olimpiki katika mbio za mita 1,500 za kina dada Faith Chepng’etich aliandikisha kasi ya juu mwaka huu akihifadhi taji la riadha za Diamond League duru ya Eugene, Amerika, Jumamosi.

Chepng’etich, 28, alikamilisha umbali huo kwa dakika 3:52.59 na kuwalemea wapinzani wake wa karibu Gudaf Tsegay kutoka Ethiopia (3:54.21) na Gabriela Debues-Stafford kutoka Canada (3:58.62) katika kitengo hicho kilichovutia watimkaji 17 akiwemo bingwa wa duru ya Birmingham, Laura Muir kutoka Uingereza aliyemaliza katika nafasi ya 11.

Bingwa wa dunia mbio za 1,500m wanaume Timothy Cheruiyot aliridhika na nafasi ya tatu katika mbio za maili moja. Alikamilisha mbele ya Mkenya mwenzake Abel Kipsang ambaye alinyakua mataji ya 1,500m ya duru mbili za kwanza za Diamond League mijini Doha na Birmingham.

Bingwa wa dunia riadha za washiriki wasiozidi umri wa miaka 20 Vincent Keter alikamilisha katika nafasi ya 12. Wakenya waliona vumulimuli katika mbio za 3,000m kuruka viunzi na maji ambapo Celliphine Chespol na Jackline Chepkoech waliridhika na nafasi za sita na saba, mtawalia.

Rosefline Chepng’etich hakukamilisha.

Wazawa wa Kenya Norah Jeruto (Kazakhstan) na Winfred Yavi (Bahrain) walikamata nafasi mbili za kwanza mtawalia. Vincent Yator alimaliza mita 5,000 katika nafasi ya 10.

  • Tags

You can share this post!

Strathmore ni wafalme Christie 7s huku Shujaa wakiangukia...

Maskini Homeboyz wajikwaa Ligi Kuu

T L