• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Dalot arefusha mkataba wake kambini mwa Man-United hadi Juni 2028

Dalot arefusha mkataba wake kambini mwa Man-United hadi Juni 2028

Na MASHIRIKA

BEKI matata wa Manchester United, Diogo Dalot, ametia saini mkataba mpya wa miaka mitano ugani Old Trafford.

Difenda huyo raia wa Ureno amerefusha kandarasi yake kambini mwa Man-United hadi Juni 2028 huku akiwa radhi kurefusha zaidi mkataba huo kwa mwaka mwingine mmoja.

Dalot, 24, alitua ugani Old Trafford mnamo 2018 baada ya kuagana na kikosi cha FC Porto cha Ureno alichokichezea mara 107.

Nyota huyo amechezea timu yake ya taifa mara 11 na kuwajibikia Man-United mara 42 katika mashindano yote ya msimu huu wa 2022-23 chini ya kocha Erik ten Hag.

Alikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kilichotegemewa na Man-United kukomoa Newcastle United kwenye fainali ya Carabao Cup mnamo Februari 2023. Taji hilo lilikuwa la kwanza kwa Man-United kuzoa tangu mwaka wa 2017.

Alitegemewa pia na Man-United kwenye nusu-fainali ya Kombe la FA dhidi ya Brighton ambapo mshindi aliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti. Ushindi huo dhidi ya Brighton uliwakatia tiketi ya kuvaana na Manchester City kwenye fainali ya Kombe la FA ambayo itasakatwa mnamo Juni 3, 2023 ugani Wembley.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Omanyala atutumua misuli akijiandaa kuwakabili wapinzani...

Sevilla wakomoa AS Roma kwa penalti na kunyanyua taji la...

T L