• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
EPL: Saka na Nketiah wabeba Arsenal dhidi ya Nottingham Forest

EPL: Saka na Nketiah wabeba Arsenal dhidi ya Nottingham Forest

Na MASHIRIKA

MABAO ya Eddie Nketiah na Bukayo Saka katika kipindi cha kwanza yamesaidia Arsenal kuanza vyema kampeni zao za EPL msimu huu kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nottingham Forest ugani Emirates.

Saka mwenye umri wa miaka 21 alifungia Arsenal bao la pili katika dakika ya 32 baada ya Eddie Nketiah kufungua ukurasa wa magoli kunako dakika ya 26.

Hata hivyo, Arsenal walilazimika kukabiliana vilivyo na Forest waliofutiwa machozi na Taiwo Awoniyi katika dakika ya 83.

Pambano hilo lilipangiwa kuanza saa nane unusu alasiri lilichelewa kwa dakika 30 kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa kutolea mashabiki tiketi za kielektroniki za mahudhurio.

Mchuano huo uliwapa Arsenal fursa ya kuwajibisha sajili wao wapya wa haiba kubwa muhula huu –  Declan Rice, Kai Havertz na Jurrien Timber aliyeondolewa ugani mwanzoni mwa kipindi cha pili kwa sababu ya jeraha.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

AFC Leopards yakubaliwa kusajili wachezaji baada ya...

Harry Kane sasa ni mali rasmi ya Bayern Munich

T L