• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya: Guardiola asipobeba taji atasaga meno

Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya: Guardiola asipobeba taji atasaga meno

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City watashuka leo Jumamosi ugani Ataturk Olympic jijini Istanbul, Uturuki, kuvaana na Inter Milan ya Italia kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Pambano hilo linatarajiwa kuwapa Man-City fursa ya kutia kapuni taji la tatu msimu huu baada ya kunyanyua Kombe la FA na Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City walitinga fainali ya UEFA muhula huu baada ya kupokeza Real Madrid kichapo cha 5-1 kwenye mikondo miwili ya nusu-fainali. Inter kwa upande wao walijikatia tiketi ya fainali baada ya kukomoa AC Milan 3-0 katika michuano ya mikondo miwili ugani San Siro.

Mechi yao leo pia inampa Guardiola jukwaa mwafaka zaidi la kujinyanyulia taji la UEFA kwa mara ya kwanza tangu abanduke kambini mwa Barcelona mnamo 2012 akijivunia kuzoa jumla ya mataji 14.

Hadi kufikia msimu wa 2020-21, Guardiola hakuwa amefaulu kufikisha Man-City zaidi ya hatua ya robo-fainali za UEFA licha ya kujiunga na kikosi hicho mnamo 2016.

Chelea waliwakomoa 1-0 katika fainali ya UEFA mnamo 2021 katika uwanja wa Estadio do Dragao jijini Porto, Ureno, kabla ya Real Madrid kuwadengua kwenye nusu-fainali za 2021-22.

Tangu Man-City watandike Real, miamba hao walifanikiwa kuhifadhi taji la EPL kwa alama 89 kabla ya kunyakua Kombe la FA kwa mara ya pili chini ya Guardiola aliyewaongoza kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza mwaka wa 2009.

Mechi dhidi ya Man-United ilikuwa ya tatu kati ya saba kwa Man-City kushinda ugenini. Awali, miamba hao walikuwa wameshindwa kutamba dhidi ya Real na Bayern ugenini kabla ya kuangushwa pia na Brentford kwa 1-0 mnamo Mei 28, siku tatu baada ya Brighton kuwalazimishia sare ya 1-1 katika EPL ugani Amex.

Hata hivyo, Man-City wamefunga katika kila mojawapo ya mechi saba zilizopita za UEFA na huenda wakaweka rekodi ya kuwa kikosi cha nne kutoka Uingereza kuwahi kujitwalia taji la UEFA.

Miezi minne baada ya kutandika Milan 3-0 katika gozi la Supercoppa Italiana, Inter walikomoa tena kikosi hicho kwenye nusu-fainali ya UEFA na kutinga fainali kimtindo.

Safu yao ya mbele itategemea pakubwa maarifa ya Lautaro Martinez anayehusishwa pakubwa na Real iwapo waajiri hao wa kocha Carlo Ancelotti watakosa kumsajili mshambuliaji mahiri wa Tottenham Hotspur, Harry Kane.

Inter ambao ni mabingwa mara mbili wa UEFA, hawajawahi kunyanyua taji la kipute hicho kwa misimu 13 tangu watandike Bayern 2-0 mnamo 2010 jijini Madrid, Uhispania.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Dereva Takamoto Katsuta alenga kumakinika kwenye mbio za...

Ruto, Raila wapongeza Faith Kipyegon kwa kuweka rekodi mpya...

T L