• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 11:20 AM
Fountain Gates ya TZ yamsajili mshambulizi Topister Situma wa Harambee Starlets

Fountain Gates ya TZ yamsajili mshambulizi Topister Situma wa Harambee Starlets

NA TOTO AREGE

TIMU ya soka ya wanawake ya Fountain Gates Princess ya Tanzania, imemsajili mshambulizi wa Harambee Starlets Topister Situma kwa muda usiojulikana.

Situma anajiunga na Fountain Gates akitokea Simba Queens ya Tanzania baada ya kuvunja mkataba na klabu hiyo. Fountain kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii imetangaza taarifa hiyo.

“Situma anasifika kwa kuzititiga nyavu ambapo amefanya hivyo akiwa na timu ya taifa ya Kenya. Pia alitesa akiwa na klabu ya Buja Queens ya Burundi ambapo alifunga magoli manne katika dimba la Mashirikisho ya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) nchini Uganda mwezi Agosti,” ujumbe huo ulisema.

Fountain pia ni nyumbani kwa wachezaji wa Starlets kama Monica Chebet, Winfrida Seda, Inviolata Mukosh na Myline Awuor.

Mchezaji huyo wa zamani wa Vihiga Queens Ligi Kuu ya  Wanawake ya Shirikisho la Soka nchini (FKF-WPL), alishinda Kiatu cha Dhahabu msimu wa 2021/22. Alifunga mabao 18.

Situma ni miongoni mwa washambulizi katika kikosi cha muda cha Starlets ambacho kiliitwa kambini na kocha Beldine Odemba, kwa maandalizi ya mechi za mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2024.

Kikosi hicho cha wachezaji 30, kinatarajiwa kuingia kambini jijini Nairobi kuanzia Jumapili.

  • Tags

You can share this post!

Zuchu adai Diamond ndiye mwanamume wa kwanza kumpa burudani...

Nondies, Kabras na KCB waingia 8-bora katika duru ya...

T L