• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Gaspo Women na Vihiga Queens wadhihirisha wako viwango vingine

Gaspo Women na Vihiga Queens wadhihirisha wako viwango vingine

NA AREGE RUTH

VINARA wa ligi Gaspo Women na Vihiga Queens wanaendelea kuonyesha ushindani mkali Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) baada ya kushinda mechi zao Jumatano.

Gaspo waliwazaba majirani wao Thika Queens mabao 4-2 katika Uwanja wa kaunti ndogo ya Thika, huku Vihiga Queens wakiilaza Ulinzi Starlets mabao 2-0 katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi.

Anita Namata alifungia Vihiga bao la kwanza dakika ya 17 kabla ya fowadi mzoefu Janet Moraa kufunga bao dakika tano baadaye.

Ushindi huo ulifanya Vihiga kufikisha alama 46, sawa na viongozi Gaspo Women ambao wana tofauti ya mabao ya juu zaidi.

Katika uwanja wa Thika, Elizabeth Wambui alifunga mabao mawili dakika ya 25 na 27 huku Diana Wacera na Lydia Akoth pia wakilenga shabaha dakika ya 29 na 49.

Stella Odhiambo alikuwa ameipatia Thika bao la kuongoza dakika ya tano huku Pauline Musungu akifunga la pili dakiak ya 40.

Uwanjani Camp Toyoyo jijini Nairobi, Zetech walitoka sare ya 1-1 na Trans Nzoia Falcons.

Falcons walikuwa wa kwanza kuchka na wavu dakika ya 13 kabla ya fowadi wa Zetech Abudala Firidhaus kusawazisha dakika za lala salama za kipindi cha pili.

Katika mechi nyingine iliyoandaliwa katika uwanja wa ASK katika kaunti ya Nakuru, Nakuru City Queens ilimenyana na Wadadia Women kwa sare ya 3-3.

Mshambulizi wa Nakuru Lena Were alifunga mabao mawili dakika ya 45 na 70 mtawalia huku Merceline Wafula akifunga moja dakika ya 76.

Kwa upande wa Wadadia, Jackline Chesang’ alifunga bao lake la 11 msimu huu dakika ya 46 kabla ya Mukwana Eglay kufunga mabao mawili dakika ya 84 na 90.

Kisumu All Starlets walipata alama za bure na mabao mawili baada ya wenyeji Kangemi Ladies FC kukosa kufika ugani Dagoretti High.

Ratiba ya Alhamisi

Kayole Starlet FC vs Bunyore Starlets FC (Camp Toyoyo, Nairobi 3pm)

  • Tags

You can share this post!

Yesu wa Tongaren msalabani kuhusu mafunzo yake

Serikali yakiri ugumu wa kudhibiti madhehebu

T L