NA CHARLES ONGADI
GOOD Hope FC iliimarisha kampeni ya kuhifadhi taji la Ligi ya Mombasa Premier kwa kuilaza Mvita Youngsters 2-0 katika shule ya sekondari ya Khadija, Kisauni, mnamo Jumamosi, Septemba 16, 2023.
Ali Abdulkadir alitinga bao la kwanza dakika ya 24 kabla ya Issa Ibrahim kudungilia msumari wa mwisho dakika ya 76.
Katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Mvita Youngsters iliikung’uta Good Hope 1-0 katika shule ya msingi ya Mvita.
Kocha wa Good Hope Shem ‘Otti’ Lumumba aliwapongeza sana wachezaji wake kwa ushindi na kuonya timu pinzani.