• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 7:55 AM
Harambee Starlets warejea kimya kimya baada ya kukosa fursa ya kukwachua Sh15m katika WAFCON

Harambee Starlets warejea kimya kimya baada ya kukosa fursa ya kukwachua Sh15m katika WAFCON

NA TOTO AREGE

Baada ya timu ya taifa ya Kenya ya wanawake Harambee Starlets kuondolewa kwenye mashindano ya kufuzu Kombe la Wanawake la Mataifa ya Afrika (WAFCON), siku ya Jumatano Desemba 6, 2023, walirejea nchni kimya kimya.

Kenya iliondolewa kwenye mashindano hayo na timu ya The Mares ya Botswana ambao waliwanyorosha kwa jumla ya alama 2-1.

Tayari timu 12 sasa zimejikatia tiketi ya kushiriki katika mashindano hayo ambayo yataandaliwa nchini Morocco mwakani.

Lakini, hivi Starlets ingeweza kupata faida kiasi gani kama ingefanikiwa kufuzu?

Kulingana na orodha ya zawadi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Starlets ya mkufunzi Beldine Odemba ingeweza kupata Sh15,335,000 kwa kufuzu tu.

Kwa bahati mbaya, Kenya ambayo ilishiriki WAFCON kwa mara ya kwanza 2016, iliiondoa Indomitable Lionesses ya Cameroon katika hatua ya kwanza kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya mechi hiyo kuishia sare ya 1-1.

Huku Kenya ikijutia fursa iliyopotea baada ya kupoteza penalti za (Violet Nanjala huko Nairobi na Cynthia Shilwatso huko Gaborone), Botswana, Tanzania, Mali, Zambia, Senegal, Tunisia, DR Congo, Ghana, Algeria, mabingwa watetezi Afrika Kusini na washindi mara 11 Nigeria walijiunga na Morocco katika mashindano hayo ya timu 12.

Mshindi nchini Morocco atapata Sh76,430,000 na mshindi wa pili Sh45,858,000.

Timu nne zitakazotolewa katika robo fainali zitapata Sh26,750,500 kila moja. Mshindi wa tisa amehakikishiwa Sh22,929,000, wakati timu tatu za mwisho zitapata Sh15,335,000 kila moja.

Kenya ambao ni washindi wa mashindano ya CECAFA ya mwaka 2019, walikuwa wameahidiwa Sh5 milioni na Waziri wa Michezo Ababu Namwamba ikiwa wangefuzu kwa mashindano hayo.

Orodha ya mwisho ya washiriki wa WAFCON ya 2024 ilithibitishwa baada ya raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu siku ya Jumanne, ambapo Ghana, ambao wamefuzu mara tatu, wamerejea baada ya kukosekana kwa miaka sita.

DR Congo wamefuzu kwa mara ya kwanza tangu 2012, na Tanzania walishiriki mara ya mwisho mwaka 2010.

Washindi mara mbili Equatorial Guinea walikuwa miongoni mwa washindwa wakubwa pamoja na Cameroon, washiriki mara nne katika hatua ya kufuzu.

Sasa, kwa timu zote 12 zilizofuzu, tahadhari inaelekezwa kwenye droo ya mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka.

Macho yote sasa yataelekeza katika mashindano ya wasichana ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 15  ya Kanda ya Kufuzu kwa Mashindano ya Soka ya Shule ya Kiafrika ya CAF ambayo yataanza Jumapili jijini Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Machogu: Usahihishaji KCPE ulikuwa kazi safi na wakuu wa...

Man U wafufuka, majirani zao Man City wakififia EPL

T L