• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 12:43 PM
Inter Milan wapepeta AC Milan na kutia guu moja ndani ya fainali ya UEFA

Inter Milan wapepeta AC Milan na kutia guu moja ndani ya fainali ya UEFA

Na MASHIRIKA

KATIKA mechi iliyosubiriwa kwa wiki kadhaa nchini Italia na kuhudhuriwa na zaidi ya mashabiki 80,000, Inter Milan walijiweka pazuri kufuzu kwa nusu-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) baada ya kupokeza AC Milan kichapo cha 2-0, Jumatano usiku.

Bao la Edin Dzeko katika dakika ya nane lilinyamazisha mashabiki wa Milan kabla ya kiungo wa zamani wa Arsenal, Henrikh Mkhitaryan, kupachika wavuni bao la pili lililochangiwa na Federico Dimarco.

Inter nusura wafunge bao la tatu kupitia kwa Hakan Calhanoglu aliyeshuhudia kombora lake likigonga mwamba.

Mshindi kati ya Inter na Milan baada ya mikondo miwili atakutana na Real Madrid au Manchester City kwenye fainali ya UEFA muhula huu.

Ingawa Inter ni mabingwa mara tatu wa European Cup au UEFA, hawajawahi kutinga fainali ya kipute hicho tangu watawazwe wafalme mara ya mwisho miaka 13 iliyopita.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Wanaotafuta jamaa wasema ngoja ngoja yaumiza

Ukora wa serikali za kaunti kudumisha vibarua wafichuka

T L