• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
JKT Queens wadhihirisha ndio malkia wa kweli CECAFA baada ya kutandika CBE

JKT Queens wadhihirisha ndio malkia wa kweli CECAFA baada ya kutandika CBE

NA TOTO AREGE

TIMU ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Queens kutoka Tanzania, itawakilisha Mashirikisho ya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF) nchini Cote d’Ivoire mwezi Novemba 2023.

JKT Queens walipata tiketi ya moja kwa moja baada ya kuinyeshea CBE ya Ethiopia mabao 5-4 katika ya penalti baada ya kuambulia sare katika fainali iliyochezwa ugani Fufa Technical Center (FTC) mjini Njeru, Uganda, Jumatano.

Hakuna yeyote aliyeona lango la mwenzake muda wa kawaida na hata baada ya kucheza dakika 30 zaidi.

Awali katika uwanja huo, Vihiga Queens walimaliza kwenye nafasi ya nne katika mashindano hayo baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Buja Queens ya Burundi katika uwanja huo.\

Timu tisa ambazo zilishiriki mashindano hayo, ziligawanywa kwenye makundi mawili. Kundi A lilihusisha timu tano huku Kundi B likiwa na timu nne pekee.

  • Tags

You can share this post!

Wanagofu 280 kuwania taji la Legendary uwanjani Ruiru

Iwapo ukeketaji ni dawa, basi mbona michepuko kwenye ndoa?

T L