• Nairobi
  • Last Updated October 1st, 2023 9:40 PM
KWPL yapamba moto mechi za msimu zikikaribia kukamilika

KWPL yapamba moto mechi za msimu zikikaribia kukamilika

NA AREGE RUTH

ZIMESALIA mechi nne nne Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) kukamilika na ushindani mkali unaendelea kushuhudiwa kwenye msimamo wa ligi kati ya Vihiga Queens, Gaspo Women na wanajeshi wa Ulinzi Starlets.

Kileleni mwa jedwali, Gaspo Women na Vihiga Queens wanaongoza katika nafasi ya kwanza na pili mtawalia wakiwa na alama 43 kila mmoja. Ulinzi inafunga tatu bora na alama 38.

Kwenye mechi ya Jumatano, Gaspo itakabiliana na mabingwa watetezi Thika Queens katika uwanja wa Manispaa ya Thika jijini Nairobi. Vihiga nao wana kibarua kigumu dhidi ya wanajeshi wa Ulinzi Starlets katika uwanjani Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi.

Wakati uo huo, aliyekuwa kocha wa Thika Fredrick Majani ameachana na timu hiyo baada ya kuitimikia kwa miezi mitatu.

“Niliondoka kwenye timu kabla ya mechi yetu dhidi ya Wadadia Women. Sijalipwa kwa muda, niliondoka kutokana na ukosefu wa mishahara,” alisema Majani.

Kulingana na mwenyekiti wa timu hiyo Fredrick Chege, aliyekuwa kocha wa timu hiyo Benter Achieng amepewa majukumu ya kunoa timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.

Kwenye mechi nyingine leo, Zetech watawakaribisha Trans Nzoia Falcons ugani GEMS Cambridge.

Mshambulizi wa Zetech Puren Alukwe ndiye atakuwa anaangaziwa sana kwenye mechi hii, baada ya kuchangia mabao mawili katika ushindi wa 4-3 wikendi iliyopita dhidi ya Nakuru City Queens

Kwa sasa anaongoza kwenye jedwali la wafungaji bora na mabao 14 sawa na mshambulizi wa Bunyore Starlets Airin Madalina. Wendy Atieno (Thika Queens) na Monicah Etot (Kisumu All Starlets) wanafuata nafasi ya tatu na nne na alama 13.

Katika uwanja wa Maonyesho ya Kilimo (ASK) mkini Nakuru, Nakuru City Queens watawaalika Wadadia Women.

Kangemi Ladies watakuwa wenyeji wa Kisumu All Starlets katika uwanja wa shule ya upili ya wavulana ya Dagorretti jijini Nairobi.

Kayole Starlets nao wataumiza nyasi dhidi ya dhidi ya Bunyore ugani Camp Toyoyo, Nairobi.

Ratiba ya mechi

Jumatano

Ulinzi Starlets FC – Vihiga Queens FC (Ulinzi Sports Complex, Nairobi 12:00 pm)

Thika Queens FC – Gaspo Women FC (Thika Stadium, Thika 12:00 pm)

Zetech Sparks FC – Trans Nzoia Falcons FC (GEMS Cambridge, Nairobi 11:00 am)

Nakuru City Queens FC – Wadadia FC (Uwanja wa Maonyesho wa ASK, Nakuru 12:00 pm)

Alhamisi

114 Kangemi Ladies FC – Kisumu All Starlets FC (Dagoretti High, Nairobi 12:00 pm)

Kayole Starlet FC – Bunyore Starlets FC (Camp Toyoyo, Nairobi 3:00pm)

  • Tags

You can share this post!

Gavana Waiguru apambana kumiliki nyumba ya Sh200 milioni  

Hatimaye wanahabari waruhusiwa kushuhudia operesheni ya...

T L