• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 6:55 AM
Lacazette abeba Lyon dhidi ya Montpellier katika Ligue 1

Lacazette abeba Lyon dhidi ya Montpellier katika Ligue 1

Na MASHIRIKA

ALEXANDRE Lacazette alifunga mabao manne, ikiwemo penalti ya dakika ya 100, katika ushindi wa 5-4 uliosajiliwa na waajiri wake Olympique Lyon dhidi ya Montpellier katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), Jumapili.

Baada ya Lacazette kufungulia Lyon ukurasa wa mabao, Elye Wahi alifungia Montpellier mabao manne bila jibu na kufanya mambo kuwa 4-1 kufikia dakika ya 55.

Hata hivyo, mabao kutoka kwa Lacazette na Dejan Lovren yalipunguza pengo hilo na Lacazette akasawazisha mambo kunako dakika ya 82.

Fowadi huyo wa zamani wa Arsenal alipachika wavuni bao la ushindi kwa upande wa Lyon sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa.

Lyon walipewa mkwaju wa penalti katika dakika ya nane ya muda wa majeruhi baada ya teknolojia ya VAR kubainisha kwamba Christopher Jullien aliangusha Lacazette ndani ya kijisanduku.

Ushindi huo ulidumisha Lyon katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa jedwali la Ligue 1 kwa alama 56 sawa na Rennes. Montpellier kwa upande wao sasa wanakamata nafasi ya 12 kwa pointi 43. Zimesalia mechi nne pekee kabla ya kampeni za Ligue 1 msimu huu kutamatika rasmi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mhubiri Ezekiel akimbilia mahakama izime agizo la kufungwa...

UEFA: Je, taji la Copa del Rey litaipa nguvu Real Madrid...

T L