• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Ligi ya Saudi Arabia itakuwa tano-bora karibuni – Ronaldo

Ligi ya Saudi Arabia itakuwa tano-bora karibuni – Ronaldo

NA MASHIRIKA

RIYADHI, Saudi Arabia

SUPASTAA Cristiano Ronaldo amedai kuwa Ligi Kuu ya Soka ya Saudi Arabia imo mbioni kuwa mojawapo ya tano-bora duniani.

Mshambulizi huyo alifungia Al Nasr bao la ushindi ikipepeta Al Shabab 3-2 mjini Riyadh hapo Mei 23 na kuweka hai matumaini madogo ya klabu hiyo nambari mbili kunyakua taji.

Mreno huyo sasa amedai kuwa ligi hiyo itakuwa miongoni mwa tano-bora hivi karibuni.

“Ligi ya Saudi Arabia inaendelea kuwa kubwa na hata mwaka ujao itakuwa bora zaidi. Hatua moja baada ya nyingine na nadhani ligi hii itakuwa miongoni mwa tano-bora duniani, ingawa inahitaji muda, wachezaji na miundombinu. Naamini taifa hili lina uwezo na ligi itakuwa kubwa,” akasema Ronaldo, 38.

Lionel Messi, Sergio Busquets na Jordi Alba ni baadhi ya masupastaa wanaosemekana wako mbioni kujiunga na timu katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Kwa sasa, hata hivyo, tovuti ya soccerprime.com inaorodhesha ligi bora duniani kuwa Uingereza (Premier League), Uhispania (La Liga), Italia (Serie A), Ujerumani (Bundesliga), Ufaransa (Ligue 1), Brazil (Brasileiro Serie A), Ureno (Primeiro Liga) na Urusi (Premier League) katika usanjari huo.

Hakuna Saudi Arabia katika 20-bora kwenye tovuti hiyo kumaanisha kibarua kikubwa kipo cha kufanywa kabla ya madai ya Ronaldo kutimia.

  • Tags

You can share this post!

Manchester United wafuzu kucheza michuano ya Klabu Bingwa...

Sheikh alalamikia kuitwa mchawi kufuatia mzozo wa mali ya...

T L