• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Madereva 34 waingia WRC Safari Rally tayari kuonyeshana ubabe Juni

Madereva 34 waingia WRC Safari Rally tayari kuonyeshana ubabe Juni

Na GEOFFREY ANENE

MADEREVA 34 kutoka mataifa 19 wamethibitisha kuwania taji la duru ya dunia ya mashindano ya mbio za magari za Safari Rally mnamo Juni 22-26 katika eneobunge la Naivasha katika kaunti ya Nakuru.

Katika makala hayo ya 70 yatakayoanzia katika bustani ya Uhuru mjini Nairobi na pia mkondo mmoja kufanyika katika kituo cha kimataifa cha michezo cha Kasarani,

Kenya inawakilishwa na madereva 12 akiwemo bingwa wa taifa Karan Patel na mshindi wa zamani wa Safari Rally Carl Tundo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati andalizi ya Safari Rally, Carl Tundo. Timu ya M-Sport Ford ilitangaza magari matatu kuingiza magari matatu katika kitengo cha P1 mnamo Mei 22 inayoongozwa na bingwa wa dunia 2019 Ott Tanak kutoka Estonia, Mfaransa Pierre Louis Loubet na Mgiriki Jourdan Serderidis. Madereva hao watapaisha Ford Puma Hybrid R1. Timu hiyo pia inajumuisha Mgiriki Georgios Vasilakis katika Ford Fiesta R2 katika kitengo cha Rally 2.

Dereva Thierry Neuville anayeongoza timu ya Hyundai, atashirikiana na Mhispania Daniel Sordo na raia wa Finland Esapekka Lappi waliokamata nafasi ya pili na tatu kwenye duru ya dunia ya Ureno, mtawalia.

Tanak, ambaye alishinda duru ya Uswidi mwezi Februari, kwa sasa ni nambari mbili kwa jumla msimu huu kwa alama 81, pointi 17 nyuma ya Rovanpera.

Timu ya Toyota Gazoo Racing Team ilishinda Safari Rally mwaka 2021 na 2022. Ina magari manne yanayoendeshwa na  Rovanpera (bingwa mtetezi), Muingereza Elfyn Evans, bingwa mara nane wa dunia  Mfaransa Sebastien Ogier na Mjapani Katsuta Takamoto in the all-conquering Yaris GR.

Raia wa Canada, Jason Bailey na James Willets wako katika kitengo cha R3. Ataendesha gari la Ford Fiesta. Atawania ubingwa dhidi ya chipukizi kutoka Kenya McRae Kimathi, Hamza Anwar na Jeremiah Wahome watakaopaisha Ford Fiesta R3.  Diego Dominguez kutoka Paraguay pia ataendesha Ford Fiesta R3.

Safari Rally ni raundi ya saba ya dunia (WRC) mwaka huu.

Orodha ya madereva wanashiriki WRC Safari Rally 2023:

1: Kalle Rovanpera (Finland)/Jonne Halttunen (Finland) Toyota GR Yaris Hybrid Rally 1

2: Takamoto Katsuta (Japan)/Aaron Johnston (Ireland) Toyota GR Hybrid Yaris Rally 1

3: Elfyn Evans (Uingereza)/Scott Martin (Uingereza) Toyota GR Yaris Hybrid Rally1

4: Sébastien Ogier (Ufaransa)/Vincent Landais (Ufaransa) Toyota GR Yaris Hybrid Rally 1

5: Thierry Neuville (Ubelgiji)/Martijn Wydaeghe (Ubelgiji) Hyundai i20 N Hybrid Rally 1

6:  Esapekka Lappi (Finland)/Janne Ferm (Finland) Hyundai i20 N Hybrid Rally 1

7:  Daniel Sordo (Uhispania)/Candido Carrera (Uhispania) Hyundai i20 N Hybrid Rally 1

8: Ott Tanak (Estonia)/Martin Jarveoja (Estonia) Ford Puma Hybrid Rally 1

9: Pierre Louis Loubet (Ufaransa)/Nicholas Gilsoul (Ufaransa) Ford Puma Hybrid Rally1

10: Jourdan Serderidis (Ugiriki)/Andy Malfoy (Ufaransa) Ford Puma Hybrid Rally 1

11: Kajetan Kajetanowicz (Poland)/Maciej  Szczepaniak (Poland) Skoda Fabia Evo Rally 2

12: Martin Propkop (Czech)/Zden?k  Jurka (Czech) Ford Fiesta MKII Rally 2

13: Daniel Chwist (Poland)/Kamil Hellier (Poland) Ford Fiesta MKII Rally 2

14: Georgios Vasilakis (Ugiriki)/Thomas Krawzik (Uingereza) Ford Fiesta Rally 2

15: Gregoire Munster (Luxembourg)/Louis Louka (Ubelgiji) Ford Fiesta Rally 2

16:  Miguel Diaz (Ufilipino)/Rodrigo Sanjuan (Uhispania) Skoda Fabia Evo Rally 2

17: Oliver Solberg (Uswidi)/Elliot Andrew Edmondson (Uingereza) Skoda Fabia Evo, Rally 2

18: Karan Patel (Kenya) Tauseef Khan (Kenya) Ford Fiesta Rally 2

19:  Armin Kremer (Ujerumani)/Timo Gottschalk (Ujerumani) Fabia Evo Rally 2

20:  Samman Vohra (Kenya)/Gugu Panesar (Kenya) Skoda Fabia Evo Rally 2

21: Aakif Virani (Kenya)/Azhar Bhatti (Kenya) Skoda  Fabia Rally 2

22: Piero Canobbio (Kenya)/Fabrizia Pons (Italia) Hyundai NG i20 Rally 2

23: Yasin Nasser (Uganda)/Ali Katumba (Uganda) Ford Fiesta Rally 2

24:  Diego Dominguez (Paraguay)/Rogelio Panate (Uhispania) Ford Fiesta Rally 3

25: Jason Bailey (Canada)/James Willets (Canada) Ford Fiesta Rally3

26:  Jeremiah Wahome (Kenya)/Victor Okundi (Kenya) Ford Fiesta Rally 3

27:   Hamza Anwar (Kenya)/Adnan Din (Kenya) Fiesta Rally 3

28:   McRae Kimathi (Kenya)/Mwangi Kioni (Kenya) Ford Fiesta Rally 3

29: Giancarlo Davite (Italia)/Sylvia Vindevogel (Ubelgiji) Mitsubishi Lancer Evo X NR4

30:  Nikhil Sachania (Kenya)/Deep Patel (Kenya) Mitsubishi Lancer Evo X NR4

31:   Evans Nzioka (Kenya)/Absalom Aswani (Kenya) Mitsubishi Lancer Evo X NR4

32:   Minesh Rathod (Kenya)/Jamie Mavtavish (Kenya) Mitsubishi Lancer Evo X NR4

33:  Carl Tundo (Kenya)/Tim Jessop (Kenya)

34:  Josiah Kariuki (Kenya)/John Ngugi (Kenya).

  • Tags

You can share this post!

Idadi ya waliofariki Shakahola yasalia 240 upasuaji maiti...

Kiatu cha Dhahabu: Wendy Atieno na Airin Madalina...

T L