• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Maguire alivyofanya ‘ile kitu’ mara hii kwa timu ya Uingereza!

Maguire alivyofanya ‘ile kitu’ mara hii kwa timu ya Uingereza!

GLASGOW, Scotland

Kocha Gareth Southgate wa timu ya Uingereza amemtetea mlinzi Harry Maguire dhidi ya mashabiki waliomfokea vikali baada ya kujifunga bao wakipimana nguvu na Scotland, Jumanne usiku, huku akidai shutuma hizo hazifai kwa mchezaji ambaye ni miongoni mwa wanaotegemewa kikosini.

Mechi ilikuwa ya 59 Maguire aliyesaidia Uingereza kutinga nusu-fainali ya Kombe la Dunia la 2018 na fainali ya Euro 2020, lakini alifunga langoni mwake katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Scotland ugani Hampden Park.

“Mchango wa Maguire umekuwa mkubwa tangu aanze kuchezea timu hii, na kamwe hatujawahi kushuhudia mchezaji akishutumiwa hivyo. Huu ni utani mkubwa!,” alisema Southgate.

“Maguire ni miongoni mwa wachezaji wenye usoefu mkubwa kikosini na anastahili heshima ya hali ya juu. Ni mchezaji wa kiwango cha juu na tutaendelea kumutetea dhidi ya shutuma zozote.”

Maguire alipokonywa unahodha katika klabu ya Manchester United, lakini amebakia pale Old Trafford kufuatia majeraha kwa mabeki wenzake muhimu.

Alipewa nafasi kwa mara ya kwanza msimu huu mnamo Septemba 3 alipoingia United ikicheza Arsenal na kulazwa 3-0.

Dhidi ya Scotland, mlinzi huyo aliingia katika kipindi cha pili na kupokea foka za kila aina kutoka kwa mashabiki wa timu yake kabla ya kufunga langoni mwake bao dakika ya 67.

“Kamwe sijafurahia tabia ya mashabiki. Tutaendelea kumtetea licha ya makosa yaliyotokea. Ni jambo la kushangaza kwamba shutuma hizi zilitoka kwa mashabiki wetu pamoja na wajambuzi wa mechi Waingereza. Wamebuni uadui dhidi ya Maguire ambao hatutauvumilia kamwe.”

“Naelewa, hawakufurahia bao la kujifunga, lakini hatutakubalia mchezaji kushambuliwa kiasi hicho.”

Akizungmza kupitia BBC Radio 5 Live, aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Uingereza, Chris Waddle alikashifu tabia hizo za mashabiki.

“Anastahili pongezi kwa kucheza vizuri, licha ya bao la kujifunga. Lazim tuelewe ana upungufu fulani katika kuzuia mipira, lakini ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa kikosini.”

Licha ya shutuma kali, Maguire alimaliza mechi akiwa nahodha baada ya Harry Kane kutolewa dakika ya 84 baada ya kufunga bao. Mabao mengine ya Uingereza yalifungwa na Phil Foden na Jude Bellingham.

“Maguire alieleza na kuomba msmaha kutokana na kilichotokea na sharti tuheshimu aliyosema. Tulipata ushindi mkubwa. Mchango wake ulikuwa mkubwa.”

Kwingineko, Ubelgiji iliitandika Estonia 5-0 kwenye mechi ya mchujo wa kufuzu kwa Euro 2024 ambayo mshambuliaji mahiri Romelu Lukaku alifunga mabao mawili, huku mengine yakipatikana kupitia Jan Vertonghen, Leadro Trossard na Charles De Ketelaere.

Matokeo mengine yalikuwa Malta 0 Macedonia Kasakzin 2, Italia 2 Ukraine 1, Norway 2 Georgia 1, Sweden 1 Austria 3, Israel 1 Belarus 0, Uhispania 6 Cyprus 0, Romania 2 Kosovo 0, Uswizi 3 Andorra 0.

  • Tags

You can share this post!

Waliokufa katika kimbunga Libya wapita 5,000 huku zaidi ya...

Watu 6,000 waangamia baada ya kimbunga kupiga eneo la...

T L