• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
Mashabiki: Tuko na wewe Mandonga hata ikiwa watakuangamiza

Mashabiki: Tuko na wewe Mandonga hata ikiwa watakuangamiza

NA MWANGI MUIRURI

HUKU mwanabondia Karim Mandonga maarufu kama mtukazi, wa Tanzania akitarajiwa kupigana Zanzibar mnamo Agosti 27, 2023, na pia uwezekano wa kuvaana nchini Uingereza kabla ya Desemba, mashabiki wake wamezindua misururu ya kumtania mitandaoni.

Hii ni kutokana na mtindo wake mpya hasa baada ya kutandikwa mechi mbili mfululizo nchini Kenya na pia kwao Tanzania chini ya siku 10.

Baada ya kuangushwa katika raundi ya tatu na ya sita na bondia Daniel Wanyonyi mnamo Julai 22, 2023 katika ukumbi wa Sarit, Nairobi aliangushwa tena Jumamosi iliyopita eneo la Mwanza, Tanzania na mwanabondia Moses Golola.

Bw Golola wa Uganda, alihitaji raundi tatu tu kummalizia mtukazi kazi yake.

Lakini mashabiki wake wamezidi kumpa risala zao za rambirambi na licha ya wengi kumtahadharisha kwamba mbio yake kukimbizana na mechi kila wiki bila ya kujipa muda wa kujijenga upya kutamponza, walimhakikishia kwamba “tuko nawe Mandonga hadi wakuue”.

Kwa sasa, Mandonga anasema wapangaji wa mechi zake wanamwandalia majini na waganga wa kienyeji kiasi kwamba ngumi zake zinahepeshwa na paka weusi na majike mazee ukumbini, huku za wapinzani zikimdondosha kwa njia haelewi katu.

Mtukazi sasa anashuku kufanyiwa uganga kiasi cha kudondoshwa bila ya hiari yake na pia kinyume na uwezo wake wa ushujaa.

Anashuku pia uganga ulimwondoa uzani ili aangushwe katika mechi mbili alizoshiriki, sanasana akilia kuhusu Bw Golola.

“Yule bondia sijamuelewa…Ana mikoba kama mganga wa kienyeji…Kavaa migolole, ila bondia yule niliyeletewa na nikaishia kupoteza sielewi,” akasema Bw Mandonga.

Alisema kwamba atapima uzani tena ili apate uhakika kwamba yeye ni Mandonga yuleyule wa mangumi ya Sungunya na Ukraine.

“Mimi sasa hivi nitaletewa majini hata nilivyodondokadondoka sielewi yaani,” akasema.

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Handisheki yabisha hodi?

Koome atakiwa kuwataja wahusika wa sakata ya ukodishaji...

T L