• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 8:55 PM
Mechi ya Harambee Starlets dhidi ya Albania yazama

Mechi ya Harambee Starlets dhidi ya Albania yazama

NA AREGE RUTH

HARAMBEE Starlets itasubiri kwa muda mrefu kabla ya kurejea uwanjani, kufuatia kutupiliwa mbali kwa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Albania iliyokuwa imepangwa kuchezwa Aprili 11, 2023 jijini Tirana.

Kati ya wachezaji 33 waliotajwa na kocha Godfrey Oduor katika kikosi chake cha muda, wachezaji 16 wa ndani na watatu wa kigeni walikuwa tayari wameripoti kambini mwishoni mwa juma lililopita.

“Uamuzi huu umefikiwa kwa sababu ya changamoto za usafiri kufika Albania licha ya juhudi za pamoja za wote wanaohusika,” Mkurugenzi Mtendaji wa FKF Barry Otieno alisema katika taarifa.

“Hata hivyo, shirikisho linasalia kujitolea kwa maendeleo mazuri ya soka nchini Kenya na linashirikisha mataifa mengine kikamilifu. Kuna nia kwa ya kuandaa mechi nyingine ya kirafiki wakati wa mapumziko ya kimataifa ya FIFA,” Otieno aliongeza.

Kenya ilirejea katika soka ya kimataifa, wakati Harambee Stars ilipocheza na Iran katika mechi ya kirafiki mwezi Machi 28, 2023.

Mechi hiyo ambayo ilipigwa jijini Tehran nchini Iran ambapo Kenya ilipoteza mechi hiyo 2-1.

FIFA ilisimamisha Kenya mnamo Februari 2022 kutokana na kuingiliwa na serikali lakini marufuku hiyo iliondolewa Novemba mwaka jana.

Starlets ilipoteza fursa ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2022 baada ya kushindwa kucheza mechi ya kufuzu kwa mikondo miwili dhidi ya Crested Cranes ya Uganda mwaka jana.

Mechi ya mkondo wa kwanza iliratibiwa kufanyika Februari 17, 2022 jijini Kampala na marudiano Februari 22 jijini Nairobi.

Wachezaji waliokuwa kambini:

Diana Tembesi (Vihiga Queens), Phoebe Owiti (Hakkari Gucu Spor), Christine Awuor (Zetech Sparks), Lupemba Bilonda (Thika Queens), Stellah Mulongo (Nakuru City Queens), Monica Etot (Kisumu All Starlets), Maximilla Robi (Kibera Soccer ), Mercyline Anyango (Vihiga Queens), Janet Moraa (Vihiga Queens), Valentine Khwaka (Gaspo Women), Monalizer Anyango (Zetech Sparks), Cynthia Shilwatso (Kryvbas Women), Puren Alukwe (Zetech Sparks), Merceline Wayodi (Vihiga Queens) , Lorna Nyarinda (Thika Queens), Desma Nyawade (Kisped Queens), Elizabeth Wambui (Gaspo Women), Ketsia Ngaira (Ulinzi Starlets), Sheryl Angach (Ulinzi Stalets).

  • Tags

You can share this post!

Mombasa yatuzwa kwa huduma bora za afya nchini

Mlinzi akiri kuwa na bastola bila leseni

T L