• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Messi aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao bara Ulaya

Messi aweka rekodi mpya ya ufungaji mabao bara Ulaya

Na MASHIRIKA

SUPASTAA Lionel Messi aliweka rekodi nyingine ya ufungaji mabao baada ya kuchochea Paris Saint-Germain (PSG) kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Strasbourg na hatimaye kujitwalia taji la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kwa mara ya 11 katika historia na tisa chini ya miaka 11.

PSG sasa wamewapiku Saint-Etienne na Olympique Marseille waliokuwa wakishikilia rekodi ya kunyanyua mataji mengi zaidi ya Ligue 1 (10).

Bao la Messi dhidi ya Strasbourg lilimfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika ligi kuu tano za bara Ulaya kwa magoli 496, moja zaidi kuliko Cristiano Ronaldo aliyewahi kuchezea Manchester United, Real Madrid na Juventus kabla ya kuyoyomea Saudi Arabia kuchezea Al-Nassr. Messi sasa amefungia PSG mabao 32 na mechi ya Jumamosi huenda ilikuwa yake ya mwisho kambini mwa miamba wanaotarajiwa kuagana naye msimu huu.

Licha ya kusaidia PSG kuhifadhi taji la Ligue 1, Christophe Galtier hana uhakika wa kuendelea kuwa kocha wa kikosi hicho. Galtier aliajiriwa na PSG mwanzoni mwa msimu huu baada ya kuongoza Lille kutwaa ufalme wa Ligue 1 mnamo 2020-21 . Matarajio yalikuwa ashindie miamba hao ufalme wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) ila Bayern Munich ikawadengua mapema katika hatua ya 16-bora.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Seth Panyako ajiuzulu naibu mwenyekiti UDA akidai imefeli...

Seneta Onyonka: Rais Ruto yafanye magazeti kuwa rafiki...

T L