• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Mpango wa Serikali ni muhimu kwa wachezaji waliostaafu

Mpango wa Serikali ni muhimu kwa wachezaji waliostaafu

NA JOHN ASHIHUNDU

MPANGO wa kuinua maisha ya wanasoka wa zamani waliowahi kuchezea timu ya taifa Harambee Stars umepokelewa kwa furaha tele na majagina hao ambao wanaisha katika maisha ya upweke baada kufanyia taifa hili makubwa miaka iliyopita.

Waziri wa ICT, Eliud Owalo akiandamana na Waziri wa Michezo Ababu Namwamba walisema Serikali inapanga kuzindua mradi wa kusaidia wanasoka hao wastaafu ambapo baadhi yao watapewa kazi katika afisi za michezo kwenye kaunti zao.

“Wengi wa wanasoka waliong’ara miaka iliyopita wamechoka na hawana nguvu walizokuwa nazo wakati wa kusakata soka. Akili zao zinataka kufanya jambo, lakini mwili haukubali, hivyo wanahitaji usaidia wa kila aina,” alisema Owalo alipotembelea majagina wa Gor Mahia na kuwapa Sh500,000, mbali na mavazi ya mazoezi.

Kadhalika, Waziri huyo alikutana na wachezaji wa sasa wa klabu za Gor Mahia na AFC Leopards kabla ya pambano la Mashemeji Derby lililovutia mashabiki wengi wakiwemo Rais William Ruto na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, Jumapili iliyopita.

Naye Namwamba alisema baadhi ya majagina hao walipata majeraha mabaya au magonjwa yaliyowawezesha kustaafu mapema na sasa yanawasumbua na kufanya maisha yao kuwa magumu.

Reginald Asibwa wa Wazee wa Kazi wa AFC Leopards akimkaba mwenzake wa Wazee wa Gor Mahia. PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Namwamba alisema atahakikisha baadhi yao wamuajiriwa kwenye afisi za michezo kuhudumua katika majukumu tofauti, kama ukufunzi wa soka, wataalamu wa mazoezi ya viungo na hata kama wachambuzi wa habari za michezo.

Alisema waliofanikiwa kupata ajira zinazolipa vizuri kulingana utaaluma wao kama JJ Masiga, William Obwaka miongoni mwa wengine wataachwa waendelea kuendesha shughuli zao popote walipo, vile vile wanaofanya kazi kama makocha kama Bernard Mwalala, Nicholas Muyoti, Zedekiah Otieno “Zico”.

Kadhalika kuna wale waliojiunga katika siasa baada ya kustaafu, lakini kuna wengi wanaishi maisha magumu baada ya kustafu, baadhi yao wakijipata katika unywaji wa kupindukia ama dawa za kulevya na kupatwa na msongo wa maisha, hasa wale waliostafu mapema.

Wachezaji Sammy ‘Pamzo’ Omollo na Boniface Ambani wakichezea timu za wakongwe za Wazee wa Kazi Gor Mahia na Wazee wa Kazi AFC Leopards mtawalia mnamo Jumapili. PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Namwamba alisema michezo haifahi kuchukuliwa kama shughuli za burudani baada ya kazi kama ilivyokuwa miaka iliyopita, bali ni kazi kubwa inayoweza kubadilisha maisha ya vijana wengi wanaosakata kwa sasa.

Alitaka klabu zitilie mkazo makubaliano ya ajira kwa wachezaji kama walivyo wafanyakazi wengine, huku akisisitiza Serikali haipaswi kulaumiwa kwa changamoto zinazowakumba wachezaji, kwa vile lazima makubaliano ya mikata yao ifuatwe na timu wanazochezea.

Alisema kuna wachezaji wengi hasa katika mataifa ya Ulaya ambao maisha yao ni mazuri kutoka ana malipo wanayopata kulingana na mikata yao, na wamekuwa maish mazuri wakistaafu. Alisema boma au pensheni za wanamichezo ni muhimu.

  • Tags

You can share this post!

Gesora Mwasi: Kuuza bidhaa mitandaoni kwahitaji ubunifu wa...

Rais Ruto akariri kuendelea kupambana na ufisadi

T L