• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 5:50 AM
Mshambulizi Judith Atieno arefusha mkataba klabuni Rayon Sports Women

Mshambulizi Judith Atieno arefusha mkataba klabuni Rayon Sports Women

NA TOTO AREGE

MSHAMBULIZI wa Harambee Starlets Judith Atieno ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Rayon Sports Women ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini Rwanda, Taifa Spoti imethibitisha.

Mkenya huyo alikuwa anawindwa na klabu ya Simba Queens ya Tanzania baada ya kung’aa msimu jana.

Katika msimu wa 2022/23, alifungia Rayon mabao 43 katika mechi 23 na kuisaidia kupanda daraja.

Alikuwa mfungaji bora wa pili nyuma ya Mburundi Florence Imanizabayo aliyefunga mabao 60.

Atieno alipeana asisti 20 hata baada ya kukosa kucheza mechi za mkondo wa kwanza, kutokana kucheleweshwa kwa vibali vyake vya kazi.

“Rwanda sasa ni kama nyumbani mbali na kwetu Kenya. Hii ni nafasi nyingine nzuri kuisaidia timu yangu kuandikisha matokeo mazuri. Hapa ni kazi tu. Kazi kubwa ni kufunga mabao mengi kuliko msimu jana. Nataka timu yangu ichukue ubingwa, nina imani tuanweza,” Atieno ameambia Taifa Spoti mnamo Alhamisi.

Rayon walitawazwa mabingwa wa Ligi ya Daraja la Pili kwa Wanawake nchini Rwanda 2022/23 kwa mara ya kwanza kwenye historia. Kando na kutwaa ubingwa, pia walishinda kombe la Kagame Peace Cup.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mathare Women mnamo Mei 6, 2023, alituzwa kuwa tuzo mchezaji bora wa mwezi Machi. Alituzwa kikombe na vifaa vya mazoezi na hundi ya Sh13,000.

Mnamo 2018, alishinda taji la Ligi ya Divisheni ya Kwanza nchini akiwa na Mathare United Women na alikuwa mfungaji bora wa shindano hilo akiwa na mabao 37 katika mechi 30.

Mwaka uliofuata alikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo akiwa na mabao 28 katika mechi 30 lakini Mathare wakashushwa ngazi ya chini mwaka wa 2021.

Mshambulizi wa Harambee Starlets Judith Atieno 9kushoto) mwaka jana, akikaribishwa klabuni na jezi ya timu hiyo na rais wa Rayon Sports ya Rwanda Jean Fidele Uwayezu muda tu baada ya kusajiliwa na klabu hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Kemsa kuteketeza dawa za Sh1.8 bilioni zilizoharibika

Vilio vyazuka kuhusu masharti mapya ya Mpango wa Elimu...

T L