• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Murang’a wahitaji ushindi nyumbani

Murang’a wahitaji ushindi nyumbani

NA JOHN ASHIHUNDU

BAADA ya juhudi zao kuvurugwa na limbukeni Silibwet Leons mwishoni mwa wiki, Murang’a Seal italazimika iandikishe ushindi dhidi ya SS Assad katika mechi nyingine ya Supa Ligi (NSL) timu hizo zitakapokutana kesho Jumatano ugani St Sebastian Park, Kaunti ya Murang’a.

Kikosi hicho cha kocha Vincent Nyaberi kilitoka bila kufungana na Silibwet katika mechi iliyochezewa Bomet Stadium, ambapo licha ya kubakia katika nafasi ya pili, wako nyuma ya vinara Shabana kwa pointi tisa.

Shabana ambao watakuwa nyumbani ugani Gusii dhidi ya Naivas FC wanaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 51, wakifuatwa na Murang’a Seal walio na 41.

Tangu walazwe 3-1 na SS Assad mnamo Aprili 14 mjini Kwale, Shabana wameandikisha ushindi mara nne fululizo wakati wamebakisha mechi tisa kumaliza ratiba yao.

Akizungumza na Taifa Spoti baada ya mazoezi, Katibu Mtendaji wa klabu hiyo, Stephen Kiama alisema mashabiki wameahidi kujitokeza kwa wingi kushangilia kikosi katika mechi hiyo ya kesho itakayoanza saa nane alasiri.

“Tunataka kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu wakati tukilenga taji la msimu huu, mbali na tiketi ya kufuzu kwa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) baada ya kukaa nje tangu 2006,” aliongoza kiongozi huyo wa miaka mingi katika klabu hiyo.

Kwingineko, Kisumu AllStars watakuwa nyumbani ugani Moi Stadium kupigania ushindi baada kuchapwa marai tatu mfululizo.

Katika mechi nyingine, Vihiga United watazuru Nairobi kukabiliana na Darajani Gogo katika mechi itakayochezewa Camp Toyoyo, wakati Migori Youth wakialika Mara Sugar ugani Migori Stadium.

Mechi za Jumatano ni Migori Youth v Mara Sugar (Migori Stadium, saa nane), Shabana v Naivas (Gusii Stadium, saa nane), Kisumu AllStars v Silibwet Leon’s (Moi Stadium, saa nane), Darajani Gogo v Vihiga United (Camp Toyoyo, saa tisa), MCF v Mombasa Elite (Machakos, saa tisa), Murang’a Seal v SS Assad, saa tisa).

  • Tags

You can share this post!

Miili 21 yafukuliwa idadi ya walioangamia Shakahola...

Raila kortini kupinga jopo la Shakahola

T L