• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 9:50 AM
Mwanahabari maarufu wa michezo Sean Cardovillis aaga dunia

Mwanahabari maarufu wa michezo Sean Cardovillis aaga dunia

NA GEOFFREY ANENE

MTANGAZAJI wa zamani wa Shirika la Habari la Nation (NMG), Sean Cardovillis ameaga dunia.

Mwanahabari huyo mtajika wa michezo alipatikana amefariki mapema Jumamosi (Septemba 9) nje ya nyumba yake kwenye barabara ya Rhapta Road mtaani Westlands. Aliishi pekee yake.

Sean alifanya kazi na kampuni ya NMG kati ya mwaka 2014 na 2020 katika kituo cha redio na pia runinga.

Maafisa wa polisi na mashahidi wamesema kuwa mnadhifishaji katika eneo hilo alipata mwili wa Sean katika ngazi ya kuelekea katika nyumba yake kwenye orofa ya nne ya jumba hilo.

Mwanahabari huyo aliyetambulika zaidi katika michezo ya mbio za magari na raga, anasemekana alikuwa ameonekana akipeleka baiskeli kabla ya kurejea nyumbani Ijumaa karibu saa moja jioni hivi.

Polisi wanasema haijabainika wazi kama alifariki Ijumaa usiku ama Jumamosi asubuhi.

Mashahidi wamesema kuwa mnadhifishaji wa jumba hilo aliarifu wakazi wa jumba hilo kuhusu tukio hilo. Ambulensi pamoja na polisi walifika katika eneo hilo ambapo watoaji wa huduma za afya walithibitisha Sean alipatikana akiwa amekata roho.

Mwili wake ulisafarishwa kadi katika chumba cha kuhifadhi maiti. Wakati wa kufariki kwake, Sean alikuwa mtangazaji katika kituo cha habari cha Capital FM.

Mkurugenzi wa Vipindi katika Capital FM Danny Munyi amemuomboleza Sean akimtaja kuwa ni mtu aliyeelewa kazi yake.

“Tumempoteza mwanahabari hodari wa michezo,” amesema Munyi.

Alianzia utangazaji Capital FM mwaka 1997 kabla ya kuingia NMG mwaka 2014. Amefanya kazi pia katika kituo cha habari cha KTN, miongoni mwa mashirika mengine.

  • Tags

You can share this post!

Uchaguzi wa viongozi wa UDA kufanyika Desemba 2023 –...

Wanaume wawili wazuiliwa kwa kukuza bangi shambani

T L