• Nairobi
  • Last Updated December 4th, 2023 6:37 PM
Neymar alitaka kasri la vyumba 25 kabla ya kuhamia klabu ya Saudia

Neymar alitaka kasri la vyumba 25 kabla ya kuhamia klabu ya Saudia

NA MASHIRIKA

NEYMAR alitaka kasri la vyumba 25, bwawa la kuogelea na chumba cha kujituliza kwa mvuke maalum, wafanyakazi na wanane wa kusafisha nyumba, limefichua jukwaa la Kihispania la Cope.

Jukwaa hilo linaongeza kwamba Neymar alitaka magari tisa ya kifahari na mahitaji yote ya usafiri, mikahawa na hoteli yagharimiwe na wasimamizi wa klabu ya Al-Hilal.

Haijabainika wazi ikiwa matakwa ya Neymar yalitimizwa lakini unaula vizuri pale Al-Hilal, gazeti la nchini Ufaransa la L’Equipe likikadiria huenda atapokea Sh50 bilioni kwa kipindi cha miaka miwili na klabu hiyo.

Hata hivyo, Neymar bado anausoma mgongo wa Cristiano Ronaldo, anayepokea Sh32 bilioni kwa kila msimu katika klabu ya Al-Nassr.

  • Tags

You can share this post!

Mandago kizimbani kwa kashfa ya Sh1.1 bilioni

Vihiga Queens watinga nusu fainali Dimba la CECAFA

T L