• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:50 AM
Omanyala atetemesha kwenye mbio za mita 100 katika mashindano ya Zagreb Continental Gold Tour

Omanyala atetemesha kwenye mbio za mita 100 katika mashindano ya Zagreb Continental Gold Tour

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Afrika na Jumuiya ya Madola mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala ameibuka mfalme wa Boris Hanzekovic Memorial Continental Tour jijini Zagreb nchini Croatia, Jumapili.

Wiki chache baada ya kusikitisha kwenye Riadha za Dunia jijini Budapest nchini Hungary alipomaliza nafasi ya saba kati ya washiriki nane katika fainali mnamo Agosti 20, Omanyala ametwaa taji kwa sekunde 9.94.

Afisa huyo wa polisi amefuatwa kwa karibu na Oblique Seville kutoka Jamaica (10.07) na bingwa wa Olimpiki Marcell Jacobs kutoka Italia (10.08) katika nafasi tatu za kwanza.

Brandon Carnes kutoka Amerika (10.27), Mjapani Brown Sani (10.29), Mwamerika Kyree King (10.31), raia wa Jamaica Rohan Watson (10.32) na Jan Volko kutoka Slovakia (10.41) wamefuatana kutoka nafasi ya nne hadi nane (mwisho). Wote wanane walitia kapuni fedha wakiwemo watatu wa kwanza Sh722,733, Sh433,639 na Sh289,093, mtawalia.

Bingwa wa Monaco Diamond League, Omanyala sasa anaelekea katika fainali ya Diamond League mjini Eugene nchini Amerika itakayofanyika Septemba 16.

  • Tags

You can share this post!

Suala la sava za IEBC lisifike meza ya mazungumzo, Gachagua...

Ripoti ya upasuaji yabaini mwalimu aliyefariki siku chache...

T L