• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Omanyala atutumua misuli akijiandaa kuwakabili wapinzani katika Diamond League nchini Italia

Omanyala atutumua misuli akijiandaa kuwakabili wapinzani katika Diamond League nchini Italia

Na GEOFFREY ANENE

MSHIKILIZI wa rekodi ya Afrika mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala atakuwa na fursa nzuri ya kulipiza kisasi atakapokutana na Mwamerika Fred Kerley katika Diamond League mjini Florence, Italia mnamo Ijumaa.

Macho pia yatakuwa kwa malkia wa mbio za 1,500m, Faith Chepng’etich Kipyegon.

Majina makubwa kutoka Kenya katika mbio za 3,000m kuruka viunzi na maji za akina dada ni Beatrice Chepkoech, Jackline Chepkoech na Fancy Cherono. Watapimwa vilivyo na Muethiopia Sembo Almayew na Mwamerika Emma Coburn.

Beatrice ni bingwa wa zamani wa Diamond League, Afrika na dunia katika kitengo hicho, Jackline ni mshindi wa michezo ya Jumuiya ya Madola naye Cherono ni bingwa wa Jumuiya ya Madola ya chipukizi mbio za 2,000m kuruka viunzi na maji mwaka 2018.

Jacob Krop na Nicholas Kipkorir watakuwa na kibarua kigumu katika mbio za 5,000m dhidi ya wakali Joshua Cheptegei (Uganda), Mohammed Ahmed (Canada), Thierry Ndikumwenayo (Uhispania-Burundi) na Waethiopia Selemon Barega na Yomif Kejelcha, miongoni mwa wengine.

Omanyala aliridhika na nafasi ya tatu Rabat Diamond League mnamo Machi 28 baada ya Kerley na raia wa Afrika Kusini Akani Simbine kunyakua nafasi mbili za kwanza, mtawalia.

Mbali na wawili hao, Omanyala aliyeandikisha muda bora katika umbali huo duniani mwaka huu wa sekunde 9.84, atakabiliana na shujaa wake Yohan Blake (Jamaica) na Waamerika Marvin Bracy-Williams na Trayvon Bromell.

Chepng’etich anatarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa Muingereza Laura Muir na Muethiopia Axumawit.

  • Tags

You can share this post!

Madaraka Dei: Kamishna wa Trans-Nzoia awaonya watengenezaji...

Dalot arefusha mkataba wake kambini mwa Man-United hadi...

T L