• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
Omanyala kutetemesha kwenye riadha za Diamond League

Omanyala kutetemesha kwenye riadha za Diamond League

Na GEOFFREY ANENE

MSHIKILIZI wa rekodi ya Afrika mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala ametangaza kuwa yuko tayari kutetemesha kwenye riadha za Diamond League katika mataifa ya Morocco, Italia na Ufaransa kabla ya Riadha za Dunia.

Bingwa huyo wa Afrika na Jumuiya ya Madola katika umbali huo ataanza kushiriki Diamond League kwa mara ya kwanza kabisa mjini Rabat, Morocco hapo Mei 28.

Kisha, Omanyala, ambaye ni afisa wa polisi, ataelekea mjini Florence nchini Italia mnamo Juni 2 halafu mjini Paris mnamo Juni 9.

“Kiwango kimepanda. Vita vya kutafuta taji la Diamond League vimeanza sasa. Nitashiriki duru hizo kupasha misuli moto kabla ya Riadha za Dunia,” akatangaza Omanyala anayejivunia muda bora katika mbio za 100 mwaka huu; sekunde 9.84.

Ameongeza, “Zitakuwa mbio kubwa na kushuhudia kasi ya juu… kujeni mpate burudani tosha la mbio za kiwango cha juu. Mnyama kutoka Mashariki atatetemesha Magharibi.”

Omanyala, ambaye rekodi yake ya Afrika katika umbali huo ni sekunde 9.77 kutoka nambari mbili alipata kwenye mashindano ya Kip Keino Classic mwaka 2021.

Baadhi ya malengo ambayo Omanyala ameweka mwaka 2023 ni kutetemesha kwenye Diamond League na Riadha za Dunia mjini Budapest nchini Hungary mwezi Agosti.

  • Tags

You can share this post!

Sibanduki katika siasa ng’o – Uhuru

Rais Ruto aongoza mkutano wa kundi la Wabunge na Maseneta...

T L