• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
PSG wajinasia huduma za Ousmane Dembele kutoka Barcelona

PSG wajinasia huduma za Ousmane Dembele kutoka Barcelona

Na MASHIRIKA

PARIS Saint-Germain (PSG) wamemsajili fowadi matata wa Ufaransa, Ousmane Dembele, kwa Sh7.8 bilioni kutoka Barcelona.

Dembele, 26, alijiunga na Barcelona mnamo 2017 kwa Sh24.3 bilioni kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani. Alipachika wavuni mabao 40 kutokana na mechi 185 na kusaidia Barcelona kutia kibindoni mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mnamo 2018, ametia saini mkataba wa miaka mitano kambini mwa PSG ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

“Ni fahari tele kujiunga na PSG ambao nimekuwa nikitamani sana kuwachezea kwa muda mrefu. Naamini nitafurahisha mashabiki wa kikosi hiki,” akasema Dembele.

Dembele aliwahi pia kunyanyua mataji mawili ya Copa del Rey akichezea Barcelona waliorefusha kandarasi yake kwa miaka miwili mwaka jana.

Amewajibishwa na timu ya taifa ya Ufaransa mara 37 huku akipachika wavuni mabao manne. Ndiye mchezaji wa tisa kusajiliwa na PSG muhula huu. Miamba hao walitema wavamizi nyota Kylian Mbappe na Neymar kwenye kikosi kilichopepetana na Lorient hapo jana katika mchuano wa kufungua msimu mpya wa Ligue 1.

Mbappe, 24, amekuwa akivutana na PSG kuhusu mkataba mpya huku akianika matamanio yake ya kujiunga na Real Madrid ya Uhispania.

Kwa upande wake, Neymar, 31, amewataka PSG kumwachilia huku akihusishwa na uwezekano mkubwa wa kurejea Barcelona walioagana naye kwa Sh26 bilioni mnamo 2017.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

St Anthony’s, Butere waibuka mabingwa wa soka

Mutahi Ngunyi afichua jinsi Uhuru Kenyatta aliunga mkono...

T L