• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Sammy ‘Kempes’ Owino kuwania urais FKF

Sammy ‘Kempes’ Owino kuwania urais FKF

NA JOHN ASHIHUNDU

ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa kimataifa Sammy ‘Kempes’ Owino ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi ujao wa Shirikisho la Soka (FKF).

Owino ambaye ameishi nchini Amerika kwa miaka mingi alitoa habari hizi wakati kumetokea uvumi kwamba rais wa sasa wa shirikisho hilo, Nick Mwendwa anajiandaa kubadilisha katiba ili imwezeshe akalie kiti hicho kwa muda mwingine.

Nyota huyo staa aliyewahi kuchezea klabu ya Gor Mahia aliichezea Harambee Stars kwa mara ya kwanza mnamo 1978 akiwa na umri wa miaka 18.

Akihutubia wafuasi wa kandanda mapema juma hili, Owino alishutumu uongozi wa Mwendwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake, ikiwemo kutambua klabu ya Gaspo Women baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Taifa (KWPL), msimu huu.

Katika hatua yake ya kutuliza wachezaji wa timu hiyo, Owino aliwapa Sh500,000 kama tuzo ya kumaliza katika nafasi hiyo baada ya kutamatika kwa msimu wa 2022/23 wiki iliyopita.

Gaspo Women walimaliza katika nafasi ya pili, nyuma ya Vihiga Queens ambayo ilipokea zawadi ya Sh1 milioni kutoka kwa FKF.

“Wakenya wamekuwa wakipewa ahadi za uongo kwa muda mrefu. Chini ya utawala wangu hakutakuwa na tabia hii ya uongozi tena. Niliposikia habari zao, niliamua hawataenda nyumbani bure, ndipo nikuaamua kuwapa Sh500,000,” alisema Owino ambaye aliondoka Kenya kwenda Amerika mnamo 1982 baada ya kupata udhamini wa masomo ya juu.

 

  • Tags

You can share this post!

Sevilla wakomoa AS Roma kwa penalti na kunyanyua taji la...

Matano asema Tusker hawana mpango wa kumsajili Lewis Bandi...

T L