• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Shabiki sugu wa Gor na Arsenal ashinda Sh27 milioni za SportPesa

Shabiki sugu wa Gor na Arsenal ashinda Sh27 milioni za SportPesa

Na CECIL ODONGO

Mwanaume mwenye umri wa miaka 32 shabiki wa Gor Mahia na Arsenal ambaye yupo kwenye biashara ya kuuza vipuri na vyuma ndiye mshindi wa hivi punde wa Sh27 milioni za SportPesa midweek Jackpot.

Esbon Macharia ambaye anamiliki duka la kuuza vipuri na vyuma mjini Thika,  alikuwa na furaha riboribo baada ya kupokezwa Sh27,041, 645 mnamo Jumanne mchana. Macharia alipata Krismasi ya mapema baada ya kucheza kamari akitumia Sh99 na akabashiri matokeo sawa katika mechi 13 mnamo Novemba 24.

“Nimekuwa nikibashiri mechi kwa SportPesa kwa mwaka moja sasa. Nimeshinda hapo awali ila hii ndiyo pesa ya juu zaidi ambayo nimeshinda. Sikujua  kuwa nilikuwa nimeshinda mwanzoni kwa sababu sikuangalia jinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea baada ya kucheza,” akasema wakati wa kutuzwa kwake mjini Thika akiwa ameandamana na mkewe.

“Mnamo Jumamosi, SportPesa walinipigia simu kuwa nimekuwa mshindi. Nilifurahi sana na hadi leo sina maneno mengi,” akaongeza.

Macharia ambaye ni baba wa watoto watatu hapotezi wakati na tayari amepanga jinsi ambavyo atakuwa akitumia pesa hizo. Mwanzo ana nyumba ambayo ujenzi wake umefika ghorofa ya pili ambayo anapanga kumaliza.

“Nina miradi mingi inayoendelea na pesa hizi zitanisaidia kuzimaliza. Hizi Sh27 milioni  zitanisaidia pia kuwalipia wanangu karo za shule. Leo nimeamini kuwa mimi ni milionea na mchezo huu si uongo,” akasema Bw Macharia.

Macharia sasa amefuata nyayo za shabiki mwengine wa Gor Mahia Stephen Ojwang, 50 kutoka Siaya ambaye alishinda Sh23 milioni za midweek Jackpot mnamo Aprili mwaka huu. Washindi wengine wa midweek Jackpot mwaka huu ni Seth Mokua aliyeenda na Sh24, 665,485 mnamo Septemba 2.

Jackson Mutiso kutoka Kaunti ya Machakos naye alishinda  Sh20, 892,489 mnamo Juni 6

  • Tags

You can share this post!

Milio ya risasi kutulia kwa muda katika Ukanda wa Gaza

Ufisadi: EACC yalaumiwa kumulika magavana na kuipendelea...

T L