• Nairobi
  • Last Updated June 2nd, 2023 7:14 PM
Sheffield United kumwajiri kocha Slavisa Jokanovic wa klabu ya Al-Gharafa nchini Qatar

Sheffield United kumwajiri kocha Slavisa Jokanovic wa klabu ya Al-Gharafa nchini Qatar

Na MASHIRIKA

SHEFFIELD United wamefichua mpango wa kumwajiri kocha wa zamani wa Fulham na Watford, Slavisa Jokanovic, 52.

Sheffield United almaarufu ‘The Blades’ hawajakuwa na kocha wa kudumu tangu mkufunzi Chris Wilder aagane nao mnamo Machi 13, 2021.

Kocha wa kikosi cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23, Paul Heckingbottom amekuwa akishikilia mikoba ya Sheffield United tangu kuondoka kwa Wilder. Hata hivyo, alishindwa kuzuia kikosi hicho kuteremshwa ngazi kutoka Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) hadi Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) msimu huu.

Jokanovic ambaye ni raia wa Serbia, kwa sasa anawatia makali masogora wa klabu Al-Gharafa nchini Qatar. Mkataba wake wa sasa na kikosi hicho unatamatika rasmi mwishoni mwa mwezi Juni na ni matarajio ya Sheffield United kwamba tajriba yake katika soka ya Uingereza itawasaidia kurejea EPL kwa ajili ya msimu wa 2022-23.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Buffon aweka rekodi ya kuwa kipa mkongwe zaidi kuokoa...

Liverpool waajiri kocha wao wa zamani, Matt Beard