• Nairobi
  • Last Updated December 3rd, 2023 8:00 PM
Tanzia: Olesia wa Kenya Lionesses aaga dunia

Tanzia: Olesia wa Kenya Lionesses aaga dunia

Na GEOFFREY ANENE

WAPENZI wa raga wanaomboleza kifo cha mchezaji wa timu ya taifa ya raga ya wanawake ya Kenya Lionesses, Bernadette Olesia.

Olesia, ambaye aliingia Kenya Lionesses kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2018, aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi Women’s jijini Nairobi, Jumanne.

Mwanaraga huyo aliyekuza talanta yake ya raga katika klabu ya Shamas, amefariki akiwa nahodha wa klabu ya wanawake ya KCB almaarufu Northern Suburbs inayoshiriki Ligi Kuu.

Amekuwa mchezaji muhimu kwa klabu hiyo na timu ya taifa. Majukumu yake ya mwisho katika timu ya taifa yalikuwa katika Kombe la Afrika la daraja la kwanza jijini Antananarivo, Madagascar mwezi Mei 2023.

Katika dimba hilo, Lionesses waling’ata Madagascar 29-20 na Cameroon 52-3 na kupoteza 48-0 mikononi mwa Afrika Kusini wakifuzu kushiriki mashindano mpya ya dunia ya daraja la tatu (WXV3) yatakayofanyika Oktoba 2023 jijini Dubai, Milki za Kiarabu.

“Pumzika kwa amani nahodha wa Northern Suburbs Ladies, Bernadette Olesia. Tutaonana siku moja kesho akhera,” KCB imethibitisha kupitia mtandao wake.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Wengi kutoka familia maskini watakosa...

Seneta Nyutu: Mabawabu wa Del Monte huenda wametekeleza...

T L