• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Thamani ya Saka yapanda mara 5, sasa kutia mfukoni Sh2.5 bilioni kila mwaka

Thamani ya Saka yapanda mara 5, sasa kutia mfukoni Sh2.5 bilioni kila mwaka

NA MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

THAMANI ya nyota chipukizi wa Arsenal, Bukayo Saka, imepanda mara tano ndani ya miaka mitatu.

Miaka mitatu iliyopita alikuwa na thamani ya Sh3.3 bilioni ambayo imepanda hadi Sh22.3 bilioni, kwa mujibu wa jarida la utafiti wa masuala ya soka la CIES Football Observatory.

Saka, 21, alitia saini mkataba mpya mnamo Jumatano wiki hii ili kuendelea kuchezea Arsenal hadi 2027.

Anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Kwa mujibu wa taarifa za mwandishi nguli wa soka David Ornstein, Saka atakuwa akipokea Sh2.5 bilioni kila mwaka kando na marupurupu mengine.

Kupanda kwa thamani ya staa huyo Mwingereza kunamweka kati ya wanasoka 10-bora duniani katika soka kwa mujibu wa CIES.

Ni orodha ambayo pia inajumuisha Jude Bellingham wa Borussia Dortmund ya Ujerumani na Phil Foden wa Manchester City ya Uingereza.

Mchezaji mwingine kambini mwa Arsenal, Gabriel Martineli wa Brazil, pia anaorodheshwa miongoni mwa 20 bora katika listi hiyo; thamani yake ikiwa Sh14.8 bilioni.

Orodha hiyo inaongozwa na Vinicius Junior wa Real Madrid ya Uhispania na Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain ya Ufaransa; wote wawili wakiwa wenye thamani ya Sh37.2 bilioni kila mmoja.

Wanafuatiwa na Erling Haaland wa Man-City kisha Bellingham; hawa wawili wakiwa na thamani ya Sh29.7 bilioni kila mmoja.

Saka anafunga orodha ya tano-bora.

Pedri Gonzalez na Pablo Gavi wote wa Barcelona ya Uhispania ni namba sita na saba mtawalia; kila mmoja akiwa na thamani ya Sh22.3 bilioni.

Kwenye orodha hiyo ya 10-bora pia kuna Rodrygo Goes wa Real Madrid, Jamal Musiala wa Bayern Munich ya Ujerumani kisha Foden wa Man-City; kila mmoja ana thamani ya Sh22.3 bilioni.

  • Tags

You can share this post!

Waliokamatwa kwenye msako mkali Mukuru kufikishwa kortini...

Mabilioni kuungua Huduma ikitemwa

T L