• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Uhispania Marathon: Cheptegei wa Uganda anyemelea rekodi ya dunia ya kilomita 42 ya Kiptum, ataweza?

Uhispania Marathon: Cheptegei wa Uganda anyemelea rekodi ya dunia ya kilomita 42 ya Kiptum, ataweza?

NA GEOFFREY ANENE

MAKALA ya 43 ya Valencia Marathon yanatarajiwa kusisimua mashabiki baada ya tetesi kuwa rekodi mpya dunia ya Mkenya Kelvin Kiptum (saa 2:00:35) huenda ikaviziwa na Mganda Joshua Cheptegei kwenye mbio hizo Desemba 3, 2023 nchini Uhispania.

Ni chini ya miezi miwili tangu Kiptum atetemeshe dunia kwa kuwa binadamu wa kwanza kukamilisha mbio za kilomita 42 chini ya saa moja na dakika moja aliposhinda Chicago Marathon nchini Amerika kwa saa 2:00:35 Oktoba 8, 2023 na kufuta rekodi ya dunia ya Eliud Kipchoge ya 2:01:09.

Valencia Marathon imevutia watimkaji wa kasi ya juu, wakiwemo Kibiwott Kandie (Kenya) na Cheptegei anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za mita 10,000 ya dakika 29:11.00 aliyoweka mjini Valencia Oktoba 7, 2020.

Kandie, ambaye ni mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia mbio za 21km ya dakika 57:32 kutoka Valencia Half Marathon mwaka 2020, na mshikilizi wa rekodi za dunia mbio za mita 5,000 Chepteget, watakuwa wakishiriki mbio za 42km kwa mara ya kwanza kabisa.

Pia yupo bingwa wa Prague Marathon Alexander Mutiso kutoka Kenya anayejivunia muda bora wa saa 2:03:29 katika mbio za 42km baada ya kukamilisha Valencia Marathon katika nafasi ya tatu mwaka 2022.

Vilevile, kuna bingwa wa Olimpiki na dunia Kenenisa Bekele kutoka Ethiopia aliyekosa rekodi ya zamani ya dunia ya mfalme wa marathon Kipchoge ya 2:01:39 kwa sekunde mbili akishinda Berlin Marathon nchini Ujerumani kwa 2:01:41 mwaka 2019.

Mabingwa Sisay Lemma (London Marathon 2021) na Leul Gebresilase (Valencia Marthon 2018) kutoka Ethiopia pia wako katika orodha ya wanaume wanaopigiwa upatu kufanya vyema hapo Jumapili.

Kiptum anashikilia rekodi ya Valencia Marathon baada ya kuanza maisha ya mbio za 42km kwa kutawala makala ya mwaka 2022 kwa 2:01:53.

Kitengo cha kina dada pia kimevutia wakimbiaji stadi wakiwemo Mromania Joan Chelimo aliyebadili uraia kutoka Kenya, pamoja na Waethiopia Tsehay Gemechu na Almaz Ayana.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Naibu Gavana Kisii akabwa koo na ukoo wa Nyaribari...

Homoni za kiume huwa chache kwa wanaume wasiolala vya...

T L