• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Ushindani mkali Team Kenya nusra umfanye awakimbilie Bahrain

Ushindani mkali Team Kenya nusra umfanye awakimbilie Bahrain

Na MASHIRIKA

MNAMO 2002 Jepkosgei alikuwa katika timu iliyoelekea Jamaica kwa mashindano ya World Junior Championships, akaibuka na ushindi katika mbio za 800m baada ya kuandikisha muda wa dakika 2:00.80.

Ulikuwa ndio mwanzo wa kudhihirisha kipaji chake kimataifa, na nyota yake ilizidi kung’ara.Mwaka 2003 alienda Italia ambapo alishindana katika mbio tofauti, lakini akawa na matokeo duni. Hali ikawa vivyo hivyo 2004 na 2005 akifanyia mazoezi nchini Italia.

Jepkosgei anaeleza kuwa aliporudi nyumbani aliiamua kujiunga na taifa la Bahrain ili kuwakimbilia, lakini rais wa Chama cha Riadha (AK) wakati huo, Isaiah Kiplagat, alirarua stakabadhi zake na kumuagiza aendelee na mazoezi. “Kiplagat alikuwa kama babangu na nilipomuambia nataka kujiunga na Bahrain, alirarua karatasi zangu akasisitiza niimarishe zoezi kwa mashindano ya Madola 2006,” asema.

Bidii ya mazoezi ilizaa matunda kwani mwaka 2006 alifuzu kuwakilisha taifa katika michezo hiyo ya Jumuiya ya Madola jijini Melbourne, Australia, ambako alizoa dhahabu.Mwaka uo huo, alijizolea medali ya fedha katika Continental Cup nchini Athens, Ugiriki.

Uliofuata 2007 alikuwa katika Team Kenya kunogesha mbio za World Championships Osaka, Japan, alikoshinda dhahabu katika muda wa dakika 1:56.04 huku akimbwaga bingwa wa Morocco, Hasna Benhassi., katika nafasi ya pili (1:56.99) naye Myte Martinez kutoka Spain akatosheka na nambari tatu (1:57.62).

“Nilikuwa na uoga kabla ya mashindano lakini nikakumbuka kochi wangu akiniambia kuwa anataka kuona vidole zangu ili aone kuwa nilikuwa natia bidi kushinda. Hivyo ndivyo nilivyoshinda na hiyo ilikuwa wakati mkubwa maishani mwangu,” alisema.

Katika mashindano ya Olympics ya 2008 Beijing, Uchina, Jepkosgei alishinda medali ya fedha kabla ya kushinda fedha pia kwenye mashindano ya Mbio za Dunia kule Berlin, Ujerumani.Aliendelea kushiriki kwenye mashindano kadha hadi mwaka wa 2015 aliposhiriki Mbio za Dunia na kukosa kufika fainili ndipo akaamua kuelekea likizo kwa ajili ya kujifungua mwana wake wa kwanza.

Mwaka wa 2016 alibarikiwa na mwanawe ambaye alimpa jina Becky Olympia Jepchirchir baada ya kukosa kushiriki Mbio za Olimpiki kule Rio de Janeiro, Brazil.Hali ilikuwa vivyo hivyo 2004 hadi alipokutana na mtaalamu wa sayansi ya michezo Claudio Berardelli aliyekuwa msomi wa sayansi ya michezo na alimwezesha kukuza talanta yake zaidi.

Berardelli alikuja na ujuzi na hiyo ikamsaidia vikubwa, mwishowe akaweza kuandikisha muda wake binafsi.Mwaka wa 2005, alikuwa katika majaribio ya timu iliyokuwa inaenda Helsinki, nchi ya Finland kwa mashindano ya dunia. Alishinda lakini hakuchaguliwa kuwakilisha nchi.

Alirudi Italy kufanya mazoezi zaidi na akawa katika mashindano tofauti ambapo alifuzu.Aliporudi nyumbani, aliamua kujiunga na Bahrain baada ya kupata usaidizi.Jepkosgei alienda Riadha House, Nairobi akiwa amejihami na karatasi za kujiunga na Bahrain.

Alimpa marehemu, Isaiah Kiplagat aliyekuwa rais wa Chama cha Riadha na akazirarua karatasi hizo.“Isaiah Kiplagat alikuwa kama babangu na nilipomuambia nataka kujiunga na Bahrain,alirarua karatasi zangu akisema niendelee kufanya mazoezi ya mashindano ya commonwealth, 2006,” alisema.

Mwaka wa 2006, alipata nafasi ya kuwasilisha nchi katika mashindano ya commonwealth Melbourne, nchini Australia. Alishinda dhahabu kabla ya kushinda fedha kwa mashindano ya Continental Cup nchini Athens mwaka huo.Aliweza kufaulu 2007, alipopata nafasi ya kuwasilisha Kenya katika mashindano ya World Championships Osaka, nchini Japan.

Alishinda dhahabu baada ya kuandikisha muda wa 1:56.04 na alimshinda bingwa wa Morocco, Hasna Benhassi aliyeandikisha muda wa 1:56.99, akifuatiwa na Myte Martinez kutoka Spain aliyeandikisha muda wa 1:57.62.“Nilikuwa na uoga kabla ya mashindano lakini nikakumbuka kochi wangu akiniambia kuwa anataka kuona vidole zangu ili aone kuwa nilikuwa natia bidi kushinda

. Hivyo ndivyo nilivyoshinda na hiyo ilikuwa wakati mkubwa maishani mwangu,” alisema.Katika mashindano ya Olympics ya 2008 Beijing, Uchina, Jepkosgei alishinda medali ya fedha kabla ya kushinda fedha pia kwenye mashindano ya Mbio za Dunia kule Berlin, Ujerumani.

Aliendelea kushiriki kwenye mashindano kadha hadi mwaka wa 2015 aliposhiriki Mbio za Dunia na kukosa kufika fainili ndipo akaamua kuelekea likizo kwa ajili ya kujifungua mwana wake wa kwanza.Mwaka wa 2016 alibarikiwa na mwanawe ambaye alimpa jina Becky Olympia Jepchirchir baada ya kukosa kushiriki Mbio za Olimpiki kule Rio de Janeiro, Brazil.

You can share this post!

Robert Lewandowski mashine ya kufunga mabao

Maelfu wafurika Pwani usalama ukiimarishwa

T L