• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 1:45 PM
Vardy sasa ni mmiliki wa klabu ya soka baada ya kununua hisa za kikosi cha Rochester Rhinos nchini Amerika

Vardy sasa ni mmiliki wa klabu ya soka baada ya kununua hisa za kikosi cha Rochester Rhinos nchini Amerika

Na MASHIRIKA

FOWADI mahiri wa Leicester City, Jamie Vardy, ameingia katika orodha ya wamiliki wa klabu za soka baada ya kununua “asilimia nzuri” za hisa za kikosi cha Rochester Rhinos nchini Amerika.

Klabu hiyo iliyo na makao makuu jijini New York haijawahi kushiriki soka ya ushindani mkubwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita baada ya kufilisika na kulazima kufungua milango yake kwa wadhamini mbalimbali.

Kufikia sasa, vinara wa Rhinos hawajaamua ni ligi ipi katika soka ya Amerika ambayo kikosi hicho kitashiriki kwa ajili ya kampeni za msimu mpya wa 2021-22.

“Vardy amenunua “asilimia nzuri” ya hisa za kikosi chetu katika mojawapo ya hatua zinazotarajiwa kuchangia ufufuo mkubwa wa klabu hii baada ya kuzamishwa na panda-shuka tele katika kipindi cha miaka minne iliyopita,” ikasema sehemu ya taarifa ya Rhinos.

Vardy ambaye ni raia wa Uingereza, pia ni mmiliki wa V9 Academy ambayo hutoa mafunzo kwa wanasoka chipukizi ambao hawajapata fursa ya kudhihirisha ukubwa wa vipaji vyao katika ulingo wa soka.

Kwa sasa akademia hiyo aliyoasisiwa mnamo 2016 nchini Uingereza inajivunia zaidi ya wanafunzi 90 ambao wanapokezwa malezi ya kimsingi kuhusu taaluma ya usakataji wa kabumbu. Akademia hii humvunia Vardy takriban Sh160 milioni kwa mwezi.

Rhinos ndiyo klabu ya pekee isiyoshiriki kivumbi cha Major League Soccer (MLS) kuwahi kushinda ubingwa wa US Open Cup.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Ushindi wa kulipa kisasi wa Ulinzi Stars dhidi ya Bandari FC

Huduma za choo, bafu zarejelewa eneo la Crescent baada ya...