• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Vihiga Queens waelekeza macho yote kwa CECAFA

Vihiga Queens waelekeza macho yote kwa CECAFA

NA AREGE RUTH

KOCHA wa Vihiga Queens Boniface Nyamunyamu anasema, wanaelekeza macho yote katika mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambayo yatafanyika Julai 2023 jijini Kampala, Uganda.

Vihiga wako kileleni mwa jedwali na alama 52 na walijikatia tiketi ya kuwakilisha Kenya katika mashindano hayo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) msimu wa 2022/23 kwa mara ya nne sasa.

Jumapili, waliwalaza Nakuru City Queens 2-1 katika uwanja wa maonyesho wa kilimo ya ASK jijini Nakuru na kuwafanya kutawala ligi kwa mara nyingine wakiwa na alama 52.

Mabingwa hao watetezi, watafunga kazi ya msimu huu dhidi ya Gaspo Women wikendi hii, katika uwanja wa GEMS Cambridge.

Gaspo ambao wameshikilia nafasi ya pili na alama 48 katika msimamo wa ligi, walikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa lakini wakateleza katika mechi mbili zikifuatana.

“Tulitaka sana ushindi katika mechi za mwisho za msimu na juhudi za wasichana hawa zimedhihirika wazi. Msimu huu tulipata ushindani mkali kutoka kwa wapinzani,” akasema Nyamunyamu.

“Mwaka 2022 hatukutetea ubingwa wetu nchini Tanzania kutokana na kufungiwa na FIFA. Wachezaji tegemeo walitorokea mataifa mengine na tulipata pigo kubwa. Kazi bado ipo katika mashindano ya CECAFA,” aliongezea Nyamunyamu.

Msimu jana, Vihiga walitwaa ubingwa wakiwa na pointi 60 bila kushindwa mechi yoyote. Walipata ushindi mara 19 na kupiga sare tatu bila kupoteza mechi yoyote.

Walitia mfukoni Sh 1 milioni na kikombe cha kibinafsi kwa hisani ya Kamati ya Mpito ya Shirikisho la Soka nchini (FKF) baada ya kutwaa ubingwa wa ligi.

Hata hivyo, msimu huo ulitupiliwa mbali na Kamati ya Kitaifa (NEC) ya Shirikisho la Soka nchini (FKF) ikidai kuwa haukutambuliwa na FIFA.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa wa Kamati ya Makabidhiano ya Afisi ya Gavana...

Thailand yahalalisha bhangi licha ya sheria kali za...

T L