• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 5:30 PM
Wanakriketi wa Kenya waanza Kombe la Afrika kwa kulima Rwanda

Wanakriketi wa Kenya waanza Kombe la Afrika kwa kulima Rwanda

Na VICTOR OTIENO

WENYEJI Kenya walianza makala ya kwanza ya Kombe la Afrika la kriketi ya Continent Twenty20 International (T20I) kwa kishindo, Ijumaa.

Walilemea Rwanda kwa wiketi tatu ugani Nairobi Gymkhana.

Wachezaji wa kriketi wenye zamu ya kupiga mpira walichangia pakubwa katika ushindi wa Kenya itakayokutana na Uganda katika mechi yake ya pili hapo Juni 10.

Hata hivyo, Kenya ilipoteza wiketi zake kwa haraka katika ova 10 za mwisho na kuingiza benchi ya kiufundi hofu kuwa itatupa uongozi mzuri.

Wenyeji watashukuru wapigaji wa mipira wa kwanza Rushab Patel (alama 35 kutokana na mipira 20) na Collins Obuya (alama 36 kutokana na mipira 27) naye Nelson Odhiambo akaandikisha alama 23 kutokana na mipira 24 katika ushindi huo.

Rwanda ilishinda kurusha sarafu hewani kuanzisha mechi kwa kupiga mipira kwanza.

“Tulikamata mipira ya wapinzani vyema, ingawa nadhani tunaweza kuimarika. Tulianza vyema pia upigaji wa mipira, lakini tukapotea na kutunuku wapinzani wetu wiketi rahisi. Lazima tuimarishe mchezo wetu. Naamini tutaimarika mechi zinavyokuja,” akasema Rakep Patel.

Rakep alitwikwa unahodha baada ya Sachin Bhudia kupokonywa kwa kukosekana katika vipindi vingi vya mazoezi kwa sababu ya kikazi.

Kenya itamaliza raundi ya kwanza ya mashindano dhidi ya Botswana inayonolewa na Mkenya Joseph Angara, hapo Juni 11. Timu zote zitasakata michuano tisa.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Wabunge waelekezwa kwa rimoti ya Ikulu

Kilio cha wapangaji walioahidiwa kumiliki nyumba za Buxton...

T L