• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Watford wakomoa Millwall na kupanda ngazi kushiriki Ligi Kuu ya EPL muhula ujao

Watford wakomoa Millwall na kupanda ngazi kushiriki Ligi Kuu ya EPL muhula ujao

Na MASHIRIKA

WATFORD walipanda ngazi na kurejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumamosi baada ya kuwapokeza Millwall kichapo cha 1-0 katika mechi ya Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship).

Bao la pekee na la ushindi kwa upande wa Watford lilipachikwa wavuni na Ismaila Sarr kupitia penalti baada ya fowadi huyo raia wa Senegal kuangushwa na Billy Mitchell ndani ya kijisanduku.

Watford wangalifunga mabao zaidi katika kipindi cha pili ila Mitchell akafanya kazi ya ziada na kupangua makombora mazito aliyoelekezewa na Daniel Bachmann na Mason Bennett.

Ushindi huo ulikuwa wa nane mfululizo kwa Watford kusajili katika uwanja wao wa nyumbani wa Vicarage Road.

Watford kwa sasa inakuwa klabu ya pili baada ya Norwich City kutoka Championship kupanda ngazi hadi EPL kwa minajili ya kampeni za msimu ujao wa 2021-22.

Chini ya kocha Xisco Munoz, Watford kwa sasa wanajivunia msimu wa kuridhisha zaidi ugani Vicarage Road tangu 1977. Ushindi waliousajili dhidi ya Millwall ulikuwa wao wa 18 mfululizo ugani Vicarage Road. Nusura Dan Gosling afanye mambo kuwa 2-0 mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya kushirikiana vilivyo na Tom Cleverley.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Raila atakiwa aachie Joho

Maiti ya ajuza aliyefariki 2004 hatimaye yazikwa