• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 11:30 AM
West Ham wakomoa Fiorentina na kufuzu kwa soka ya Europa League baada ya kushinda taji la Europa Conference League

West Ham wakomoa Fiorentina na kufuzu kwa soka ya Europa League baada ya kushinda taji la Europa Conference League

Na MASHIRIKA

WEST Ham United walikomesha ukame wa miaka 43 bila taji lolote la haiba kubwa kabatini mwao baada ya Jarrod Bowen kuwafungia bao la dakika ya mwisho lililowawezesha kukomoa Fiorentina 2-1 mnamo Jumatano na hivyo kujishindia taji la Europa Conference League jijini Prague, Jamhuri ya Czech.

Dalili zote ziliashiria kuwa mshindi wa pambano hilo angeamuliwa kupitia mikwaju ya penalti baada ya penalti ya Giacomo Bonaventura wa Fiorentina kufuta bao la Said Benrahma aliyewaweka West Ham kifua mbele kunakod dakika ya 62.

Mechi hiyo ilitawaliwa na hisia kali huku kwa wakati fulani nahodha wa Fiorentina, Cristiano Biraghi, akipigwa kwa chupa ya plastiki aliyotupiwa kutoka eneo la mashabiki wa West Ham.

Bao la ushindi, lilifumwa wavuni na Bowen katika dakika ya mwisho, lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Lucas Paqueta aliyeacha hoi mabeki wa Fiorentina.

Mechi hiyo ilikuwa ya mwisho kwa nahodha Declan Rice kuchezea West Ham kadri anavyohusishwa na uwezekano wa kuhamia Arsenal kwa ajili ya kampeni za muhula ujao wa 2023-24. Ufanisi wake kambini mwa West Ham ulirejesha kumbukumbu za Bobby Moore na Billy Bonds waliowahi kuongoza kikosi hicho kunyanyua mataji muhimu wakiwa manahodha.

Moore alichochea West Ham kunyanyua European Cup Winners’ Cup mnamo 1965 huku Bonds akisaidia kikosi hicho kujizolea Kombe la FA mnamo 1975 na 1980 mtawalia.

Kwa kuangusha Fiorentina, West Ham pia walifuzu kwa soka ya Europa League ambayo itawapa fursa ya kunogesha soka ya bara Ulaya kwa msimu wa tatu mfululizo chini ya kocha David Moyes; na mara ya kwanza kabisa katika historia ya klabu hiyo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Gereza la Eldoret lamulikwa kufuatia kifo cha mahabusu...

Rais Museveni athibitisha kuugua corona

T L