Habari Mseto

Migori yachagua Spika mpya

October 5th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Kaunti ya Migori ilimchagua Spika mpya kuchukua nafasi yaaliyekuwa spika Gerge Omamba ambaye amezuiwa na mahakama.

Kwenye kikao kilichofanyika kwa saa mbili ambacho mwenyekiti alikuwa spika Boaz Okoth, madiwani hao walimpigia kura Diwani wa Bukirra Mashariki Mathwe Chacha kuwa spika mpya.

Bw Omamba alijaribu bila mafanikio arudishiwe mamlaka yake ya uspika huku akijiondoa kwenye debe la kuwania uspika.

Baadhi ya madiwani wakiogozwa na Bw Omabmba walikashifu uchanguzi huo huku wakisema kwamba si halali. Bw Chacha alipata kura 41 huku madiwani 11 wakikataa kupiga kura na mpizani wake Leo Ogwanda akakosa kura.

Mvutaano unaoshuudiwa kwenye bunge hilo ulizidi wakati wa kuapishwa kwa naibu spika na hakimu mkuu wa Migori Dickson Odhiambo.

Madiwani wa bunge hilo wamekuwa na mvutano na machungu baada ya swala la kumg’oa mamalakani gavana Obado kupigwa na chama cha ODM.