Miguna adai balozi alipuuza amri ya korti

Miguna adai balozi alipuuza amri ya korti

Na RICHARD MUNGUTI

WAKILI Miguna Miguna jana alilalama vikali kwamba, Ubalozi wa Kenya nchini Ujerumani ulimnyima stakabadhi za usafiri licha ya agizo la Mahakama Kuu.

Kwenye ujumbe katika mtandao wa Twitter, Dkt Miguna alisema Balozi wa Kenya Tom Amolo alitoroka punde tu alipowasili afisini mwake.Alidai Bw Amolo aliwaambia wafanyakazi wa ubalozi huo- Bi Emmah Mabinda, Bw Kaluma na Bi Esther Mungai- wangepoteza kazi zao ikiwa wangempa stabadhi za usafiri ilivyoagizwa na mahakama.

Alisema Bi Mabinda alimweleza hajapokea maagizo kutoka Nairobi kutekeleza amri ya mahakama.“Alinitaka kudhihirisha Uraia wangu ndipo nikamwonyesha kitambulisho changu kisha akaniitisha cheti cha kurejeshewa uraia,” Dkt Miguna alidokeza.

Awali mahakama kuu iliamuru ubalozi huo umpe stakabadhi za usafiri.Ilimtaka Bw Miguna apate visa kutoka Ubalozi wa Kenya katika muda wa saa 72 ili akubaliwe kuabiri ndege itakayosafari kutoka Berlin, Ujerumani hadi Nairobi.

Mahakama iliamuru shirika la Ndege la Air France limsafirishe Miguna hadi Nairobi akiikabidhi hati halali za usafiri.Akitoa uamuzi kuhusu ombi la Bw Miguna, Jaji Ong’udi alisema Bw Miguna yuko na uraia wa nchi mbili na anahitajika kupata Visa ili aruhusiwe kusafiri Kenya.

Jaji Ong’udi alisema, “nimezingatia ushahidi wote uliowasilishwa na mawakili wa mlalamishi (Miguna). Namwamuru mlalamishi apate Visa kutoka kwa Ubalozi wa Kenya nchini Berlin ili aruhusiwe kuabiri ndege kurudi Kenya.

Yeye yuko na uraia wa nchi mbili Kenya na Canada.”

You can share this post!

STEVE ITELA: Wadau washirikiane kutatua changamoto za makao...

Wachezaji wa EPL na WSL watamalaki orodha ya wawaniaji wa...

T L