Miheso aokoa Kenya Police, Homeboyz ikipaa kileleni mwa ligi

Miheso aokoa Kenya Police, Homeboyz ikipaa kileleni mwa ligi

CECIL ODONGO na ABDULRAHMAN SHERIFF

WINGA Cliftone Miheso jana alifunga mabao mawili katika dakika za ziada na kuisadia Kenya Police kuduwaza Kariobangi Sharks 3-1 ugani MISC Kasarani.

Katika mechi nyingine, Nzoia Sugar iliagana sare tasa dhidi ya wenyeji Nairobi City Stars ugani Ruaraka.Mjini Kakamega, Kakamega Homeboyz ilitoka nyuma na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Mathare United ugani Bukhungu.

Sare hiyo ilihakikisha kuwa Homeboyz inachupa hadi kileleni mwa msimamo wa jedwali kwa alama 17 baada ya mechi saba.Sharks ni ya pili kwa alama 16 ingawa imecheza mechi nane.?FC Talanta nayo iliadhibu Bidco United 2-1 katika mechi ya pili ambayo pia ilisakatwa ugani Ruaraka.

Sofapaka ambayo ilishinda Kenya Police 2-0 wikendi iliyopita, iliilemea Wazito kwa idadi sawa na mabao ugani Dawson Mwanyumba, Taita Taveta.? Ugani MISC Kasarani, Miheso alifunga bao dakika ya 91 na 93 kuipa Kenya Police ushindi huo muhimu .? Mshambuliaji Clinton Kinanga alikuwa amewapa maafisa hao wa usalama uongozi dakika ya 14 kabla ya Pattilah Omotto kuchanja mpira safi wa ikabu kusawazishia Sharks dakika ya 47 kipindi cha kwanza.

Huu ulikuwa ushindi wa pili kwa vijana wa Kocha John Bobby Ogolla ambao wamekuwa wakisuasua, huu ukiwa msimu wao wa kwanza ligini.Aidha, Sunday Mutuku alifunga bao dakika ya mwisho na kusaidia Homeboyz kuagana sare ya 2-2 dhidi ya Mathare United ugani Bukhungu.

Beki Brian Eshihanda alijifunga dakika ya 21 kuipa Mathare uongozi kabla ya Eugene Wethuli kuongeza la pili kunako dakika ya 64. ? Hata hivyo, Yema Mwana alipunguza idadi hiyo kwa kuifungia Homeboyz bao dakika 84 kisha Mutuku akasawazisha dakika ya 98.

Mohamed Sedi na Kahiro Francis walifunga mabao ya FC Talanta huku Emmanuel Mogaka akifungia Bidco United bao la kujiliwaza.?Katika mechi iliyochelewa kuanza kwa dakika 30 kutokana na ukosefu wa ambulensi, Sofapaka ilifungiwa na Lawrence Juma dakika 42 kabla ya Wazito kusawazisha kupitia Elly Asieche dakika ya 55.

Batoto ba Mungu ilipata bao la ushindi kupitia beki Maurice Owino dakika ya 55.? Hivi leo Gor Mahia itakuwa mwenyeji wa Vihiga Bullets ugani MISC Kasarani huku Ulinzi Stars wakiwa wenyeji wa Tusker uga wa maonyesho ya kilimo jijini Nakuru.

You can share this post!

Origi awakomboa Reds tena

Barcelona waaga UEFA katika hatua ya makundi baada ya...

T L