Habari MsetoSiasa

Mimi si mwandani wa Ruto – Oparanya

February 19th, 2019 1 min read

Na Ibrahim Oruko

MWENYEKITI wa Baraza la Magavana (CoG) Wycliffe Oparanya amekanusha ripoti kwamba yu miongoni mwa washirika wa karibu wa Naibu Rais William Ruto, anapojitayarisha kuwania urais mnamo 2022.

Bw Oparanya aliye pia gavana wa Kaunti ya Kakamega alitaja ripoti hizo kama uvumi unaoenezwa na mahasimu wake wa kisiasa ili kumharibia sifa.

Badala yake, alisema kwamba analenga kuwania urais ifikapo 2022, akipinga uhusiano wowote na Dkt Ruto.

Alisema kwamba wale wanaoeneza uvumi huo wanazua migwanyiko ya kisiasa isiyofaa katika eneo hilo.

Baadhi ya ripoti zimekuwa zikidai kwamba Bw Oparanya ameanza ushirika mpya wa kisiasa na Bw Ruto, akiwa pamoja na Gavana Kivutha Kibwana wa Makueni.

Ripoti hizo zilidai kwamba Bw Ruto anawatumia viongozi hao wawili kujaribu kupenyeza maeneo ya Magharibi na Ukambani na hivyo kujipatia uungwaji mkono.