Habari Mseto

Mishi Mboko ashukuru kuchaguliwa mwanachama wa tume ya huduma za bunge

May 28th, 2020 1 min read

Na MISHI GONGO

MBUNGE wa Likoni Mishi Mboko ameushukuru muungano wa Nasa na hasa chama cha ODM kwa kumpa fura ya kuwa mwakilishi wake katika Tume ya Huduma za Bunge (PSC).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari muda mfupi uliopita Mishi ameahidi kutosaliti Nasa na ODM ambao wamemwaminia kwa nafasi hiyo.

Ameahidi kutekeleza majukumu yake kikamilifu katika tume hiyo ili kuhakikisha malengo yanaafikiwa.

Muungano wa Nasa umemkabidhi Mishi wadhifa huo baada ya kumbandua Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa katika PSC.

“Kwa niaba ya watu wa Pwani ningependa kushukuru Nasa na ODM kwa kunipa wajibu,” amesema.

Mbunge huyo sasa amechukua nafasi ya Jumwa ambaye anadaiwa kuwa mwasi anayesaliti malengo ya Nasa.