Michezo

Miss BumBum hali halali, amtaka Messi aonje asali

September 17th, 2018 2 min read

NA CHRIS ADUNGO

MSHINDI wa zamani wa taji la Miss BumBum, kipusa Suzy Cortez ametishia kutikisa na kusambaratisha uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanasoka Lionel Messi na mkewe wa ndoa, Antonella Roccuzzo, 30.

Hii ni baada ya Messi, 31, kulazimika kumruhusu mwanamitindo huyo kumfikia tena

katika mtandao wake wa Instagram kufuatia shinikizo la mashabiki waliofanikisha kampeni za #UnBlockMeMessi.

Suzy ambaye anafahamika sana kwa mazoea ya kutumia ukubwa wa ghuba zake kupagawisha kisha kuwatia kishawishini wanasoka maarufu wenye hela nyingi mithili ya changarawe, alianzisha kampeni za kumtaka Messi kumpa idhini ya kumfikia kwenye mitandao ya kijamii kwa mara nyingine mwishoni mwa mwezi jana.

“Ni tija na fahari tele kwangu. Asante sana Messi kwa kuniruhusu tena kukufikia kwenye Instagram, japo kiu itazima tu ukitalii kisima. Nawapongeza nyote mlioniunga mkono,” akaandika Suzy.

Awali, Suzy alikuwa mwepesi wa kupakia mitandaoni picha zilizoonesha sehemu kubwa ya maziwa na makalio yake kisha kumtumia Messi kupitia Instagram huku akimshawishi kufanya hima na kuanza kulimenya tunda lake litakalokuwa likimsubiri kila wakati akiwafungia Barcelona bao.

Hatua ya Suzy kutafuta upya hifadhi ya penzi lake moyoni mwa Messi inajiri miezi kadhaa baada ya kipusa Antonella kutishia kumtema mumewe iwapo angeendelea kumruhusu mwanamitindo huyo kumtumia picha za uchi wake mitandaoni.

Kilichomkoroga nyongo zaidi Antonella kiasi cha kumshauri Messi kumnyima Suzy idhini ya kumfikia mitandaoni, ni hatua ya Miss BumBum kuvua nguo na kusalia uchi wa mnyama baada ya Messi kufungia Argentina mabao matatu katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Ecuador mnamo Oktoba 11, 2017 na hivyo kuchochea timu yake ya taifa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2018 nchini Urusi.

Awali akiadhimisha miaka 27 ya kuzaliwa kwake, Suzy alivua nguo kwa mara nyingine na kutoa ahadi ya kumpa Messi ‘uhondo’ wa kurina asali katika mzinga wake iwapo angaliwaongoza Argentina kutawazwa mabingwa wa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu.

Hata hivyo, kukataliwa kwake na Messi kulimshawishi kuwaendea Neymar Jr, Philippe Coutinho na Gerard Pique ambaye mkewe Shakira, 41, anamzidi kwa miaka 10 kiumri.

Mnamo 2015, Suzy alitawazwa mshindi wa Miss BumBum, tuzo ambayo hutolewa kila mwaka kwa mwanamke mwenye makalio ‘bora’ na makubwa zaidi nchini Brazil.